MASOGANGE AJISALIMISHA MAHAKAMANI

Mrembo Agnes Gerald maarufu kama Masogange mwenye umri wa miaka 28 leo amejisalimisha mwenyewe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini dar es Salaam ikiwa baada ya Mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwake kwa kushindwa kufika mahakamani hapo kwa mara kadhaa.
Mapema mwezi uliopita, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa amri ya kukamatwa kwa mshtakiwa Masogange kwa kushindwa kuhudhuria mahakamani mara mbili kusikiliza kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.
Hatua hiyo ya kutaka kukamatwa kwa Masogange ilikuja baada ya upande wa mashitaka katika shauri lililopita, kuomba mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata kutokana na mshitakiwa huyo pamoja na wadhamini wake kutofika mahakamani, licha ya kupewa onyo.
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alikubali maombi hayo na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa Masogange.
Masogange baada ya kufika Mahakamani leo na kuulizwa sababu zilizomfanya asifike kwa muda wote aliotakiwa kufika akadai kuwa amefika mahakamani hapo ila alichelewa.
Hata hivyo, wakili wa serikali Shadrack Kimaro, ameieleza mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali (PH).
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Juni 13 mwaka huu ambapo mshtakiwa atasomewa mashtaka ya awali.
Awali ilidaiwa kuwa,Masogange anakabiliwa na tuhuma za kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam kinyume cha sheria.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post