MAWAZIRI WAWILI WANAOPEWA NAFASI KUBWA KUMRITHI PROF. MUHONGO

Mei 24 mwaka huu Rais Dkt John Pombe Magufuli alimfuta kazi aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo baada ya kuwapo mwenendo usiorodhisha kwenye sekta ya madini hapa chini haswa usafirishaji wa mchanga nje ya nchi.
Rais Magufuli alimfuta kazi waziri huyo zikiwa ni saa chache tangu alipopokea ripoti ya kamati ya Prof. Mruma iliyokuwa ikichunguza kiwango cha madini kilichomo katika mchanga wa madini kwenye makontena 277 yaliyozuiwa bandarini, na baada ya kubaini madudu mengi ilipendekeza wahusika wachukuliwe hatua.
Baada ya Rais Magufuli kumfuta kazi Waziri Muhongo, bado haijafahamaika ni nani atakayejaza nafasi hiyo ambayo inaonekana kuwa ngumu kwani mawaziri kadhaa waliopita wizarani hapo hawakutoka salama.
Kwa mujibu wa Katiba, Rais anaweze kufanya jambo moja kati ya haya mawili. Moja, anaweza kuteua mtu/mbunge mwingine kushika wadhifa huo. Pili Rais anaweza kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri ili kumpata waziri anayeamini anaweza kujaza nafasi hiyo.
Kama Rais ataamua kuchukua njia ya pili ya kufanya mabadiliko madogo kwenye baraza la mawaziri, kuna wabunge wawili ambao pia ni mawaziri wanaopewa nafasi kubwa ya kumrithi Prof. Muhongo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Geroge Simbachawene ni waziri wa kwanza anayepewa nafasi kubwa ya kuongoza wizara hiyo. Sababu kubwa inayofanya aonekane yupo katika nafasi hiyo, ni kutokana na uzoefu kiasi alionaoa katika wizara hiyo.
Simbachawene ndiye waziri pekee aliyeongoza wizara hiyo kati ya mwaka 2004 hadi 2017 akatoka bila kuwa na kashfa yoyote. Mawaziri wengine kama Daniel Yona, Ibrahim Msabaha, William Ngeleja, Prof. Muhongo waliondolewa kwa kashfa mbalimbali. Simbachawene alikuwa Waziri wa Nishati na Madini tangu Januari 2015 hadi Disemba 2015 alipohamishiwa TAMISEMI.
Mwingine anayepewa nafasi ya kurithi mikoba ya Muhongo ni Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Aidan Mwaluko John Kabudi ambaye ni mbobezi katika masuala ya sheria. Sababu kubwa inayomfanya aonekane kuwa huenda akaichukua wizara hiyo, ni kutokana na dalili kuwanza kujionyesha za yeye kutekeleza baadhi ya majukumu yanayohusiana na wizara hiyo.
Juma lililopita waziri huyo alikwenda nchini Uganda kutilia saini kandarasi ya makubaliano ya ujenzi wa mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania, kazi ambayo ipo chini ya wizara ya Nishati.
Lakini pia, wadadisi wengine wa mambo wameeleza kwamba, Rais anaweza kumpandisha Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Medadi Kalemani kuwa Waziri na kuteua mtu mwingine kujaza nafasi yake.
Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini inatarajiwa kuwasilishwa bungeni Alhamsi na Ijumaa, ambapo majadala mkubwa unatarajiwa kulenga sekta ya madini hasa usafirishaji wa mchanga wa madini nje ya nchi na sheri za madini.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post