MCHUNGAJI AKAMATWA NA POLISI KWA KUOA MKE WA MUUMINI WAKE

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera jana ililazimika kuhamia kwa muda katika kanisa la kipentekoste la Huruma Katika Kristo kufuatia kuwepo madai ya Mchungaji wa kanisa hilo kuishi kinyumba na wake za waumini wake kwa kile anachodai kushukiwa na Roho Mtakatifu.
Mbali na kuishi na wake za waumini wake, Mchungaji huyo aliyefahamika kwa jina la Jafece Josephat anadaiwa kuwakatisha masomo baadhi ya wananfunzi katika Kijiji cha Nyakintuntu ambao wamejiunga na kanisa lake.
Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka aliamuru kukamatwa kwa mchungaji huyo alipofika kusikiliza sakata hilo kutoka pande zote mbili.
Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya alisema kuwa serikali itachunguza kama kanisa hilo limesajili, na ikiwa halijasajiliwa, hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa.
Mchungaji huyo na mke (Domina Damian) wa muumini wake walianza kuishi pamoja kama mke na mume kuanzia Aprili 16 mwaka huu. Sakata hilo liliibuka baada ya mume wa Domina kutaka arejeshewe mahari yake aliyokuwa ametoa kumua mwanamke huyo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post