MESSI AISAIDIA BARCELONA KUTWAA KOMBE LA COPA DEL REY

Lionel Messi ameisaidia Barcelona kuifunga Alaves magoli 3-1 na kutwaa ubingwa wa kombe la Copa del Rey kwa mara ya tatu mfululizo.

Ushindi huo ni zawadi kwa kocha wao Luis Enrique ambaye anaacha kuinoa klabu hiyo baada ya kuwa nayo kwa miaka mitatu.

Mchezaji Ibai Gomez aliachia shuti lililogonga mwamba wa goli la Barcelona kabla ya baadaye Messi kufunga goli lake la 54 katika msimu huu kwa shuti la mpira wa kuzungusha.

Hata hivyo Theo Hernandez alifunga kwa mpira wa adhabu na kusawazisha goli hilo, lakini Mbrazil Neymar alifunga goli la pili na Paco Alcacer akigongeana na Messi akatupia la tatu.
   Wachezaji wa Barcelona wakiwa katika picha ya pamoja na kombe lao la Copa del Rey
                         Kocha Luis Enrique akiwa amenyanyua juu kombela Copa del Rey
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post