MFANYABIASHARA MAARUFU MJINI MOSHI AUAWA KWA RISASI

Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi,  wamevamia na kumuua kwa risasi mfanyabiashara Godfrey Mosha akiwa eneo lake la biashara kisha kutokomea kusikojulikana.
Mauaji ya Ndosi anayejulikana zaidi kama ‘G’ na anayemiliki maduka yanayotoa huduma za miamala ya fedha pamoja na maduka ya vileo kwa bei ya jumla, yalifanywa juzi majira ya saa 1:15 usiku na watu wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi, baada ya kumvamia akiwa katika eneo lake la biashara Kiboroloni, Manispaa ya Moshi.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Hamis Issa alithibitisha kuuawa kwa mfanyabiashara huyo kwa kupigwa risasi kifuani.
“Kwenye eneo la tukiaaji hayo huko Msumbiji,  Kata ya Kiboroloni, makachero wa polisi waliokota risasi mbili zikiwa hazijatumika pamoja na maganda mawili ya risasi,” alisema Kamanda Issa.
Polisi imesema majambazi hayo hayakupora chochote katika duka hilo la kufanyia miamala ya fedha, wala kuchukua mali yake na kwamba chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika.
Mwili wa mfanyabiashara huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufani ya KCMC ukisubiri taratibu za kitabibu na mazishi.
Kufuatia mauaji hayo, Kamanda Hamisi alisema jeshi hilo linaendelea na msako mkali wa kuwatia nguvuni wahusika.
Mauaji hayo pamoja na matukio mengine ya uvamizi kwa miaka mitatu mfululizo katika mji wa Moshi, yanadaiwa kutengeneza hofu kwa wafanyabiashara.
Akizungumzia mauaji hayo, Diwani wa Kata ya Kiborloni (Chadema), Frank Kagoma ambaye amekuwa akiongoza kikundi cha ulinzi shirikishi eneo hilo alisema:
“Hiyo familia inaandamwa na majambazi. Mwaka jana walivamia duka lake la kuuza vileo ambalo linasimamiwa na mkewe na jana wamemvamia marehemu wakiwa na bunduki aina ya SMG na kumuua.”
Kagoma alisema muda mfupi baada ya mauaji hayo, alikwenda eneo la tukio na kuelezwa kuwa kuna mfanyabiashara mwingine mwanamke (hakumtaja jina) mwenye duka la vileo naye alinusurika kuuawa, baada ya kukimbia dukani kwake ili kujiokoa.
“Mimi na wenzangu tunaofanya shughuli za ulinzi kwenye kata hii ya Kiborloni tuna imani kubwa na Jeshi la Polisi kwamba watakamatwa kwa vile hata waliotekeleza tukio la kumjeruhi kwa risasi mfanyabiashara tajiri na mmiliki wa mabasi ya Machame Safari, Clement Mbowe (Menti) mwaka jana, walikamatwa.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post