MICHY BATSHUAYI AIPATIA CHELSEA UBINGWA WA EPL KATIKA DAKIKA ZA MWISHO

Timu ya Chelsea imetawazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa msimu huu, baada ya Michy Batshuayi kuwafungia mabingwa hao goli la dakika za mwisho na kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya West Brom.

Katika mchezo huo ilionekana kama kikosi cha kocha Antonio Conte kitalazimika kuchelewa kuupata ubingwa huo jana baada ya kuwekewa ngumu na West Brom kwa muda mrefu na kuwafanya kwa kiasi fulani kuchanganyikiwa.

Lakini hali ilibadilika na taji la Ligi Kuu ya Uingereza lilitwaliwa zikiwa zimebakia dakika nane za mchezo kupitia mchezaji aliyetokea benchi Batshuayi, ambaye awali alikuwa na kipindi kigumu baada ya kusajiliwa kwa kitita cha paundi milioni 33 kutoka Marseille.
          Michy Batshuayi akifunga goli pekee katika mchezo huo na kuipa ubingwa Chelsea
     Wachezaji wa Chelsea wakimrusha juu kocha wao Antonio Conte kwa furaha ya ubingwa
        Pedro akiwa amerushwa juu na wachezaji wenzake wa Chelsea katika kusherehekea ubingwa
    Wachezaji wa Chelsea wakishangilia kwa kuwaelekea mashabiki wao waliopo jukwaani
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post