MKE WA MKUU WA POLISI WA WILAYA (OCD) ALIYEUAWA AELEZEA UTATA WA KIFO CHA MUMEWE

SHARE:

MKE wa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) wa Uvinza mkoani Kigoma, Amedeus Malenge, ambaye aliuawa kikatili juzi, amesema kifo cha mume wake ...

MKE wa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) wa Uvinza mkoani Kigoma, Amedeus Malenge, ambaye aliuawa kikatili juzi, amesema kifo cha mume wake kina utata.
Akizungumza na Nipashe nyumbani kwake, Buguruni jijini Dar es Salaam, ambako ndiko msiba uliko, Mary Amedeus, alisema kifo hicho kimejawa utata kutokana na mazingira yaliyojitoleza kuhusiana na tukio hilo.
Akitaja sababu za kudhania kuwa kifo hicho ni cha utata, Mary alisema siku ya shughuli ya kumuaga binti yake (sendoff) Alhamis iliyopita, kulitokea mzozo wa kifedha ukumbini.
Alisema kamati ya maandalizi ya shughuli iliahidi kumpa mtoto fedha taslimu kama zawadi, lakini ilipofika muda wa kufanya hivyo ukumbini, mke mwenzake ambaye alikuwa ndiye mweka hazina wa shughuli hiyo hakuzitoa.
“Binafsi sikutaka kuingilia mzozo uliozuka,” alisema kwa majonzi Mary. “Nilikaa pembeni na baadaye nikaondoka kwa hiyo sikujua kama waliumaliza vipi.”
“Siku ya harusi ilipofika (Jumamosi iliyopita) huyu mwanamke hakuja na sikupata muda wa kumuuliza mume wangu waliafikianaje kuhusu zawadi ya mtoto.”
Alisema mume wake alikuja Dar es Salaam kutoka Kigoma alipo kikazi kwa ajili ya shughuli ya mtoto wao na Jumapili aliondoka Buguruni bila kueleza anakoelekea.
“Baada ya muda alinitumia fedha (kwa njia ya simu) na kuniambia ninunue umeme wa Luku na nyingine za chakula… hatukuwasiliana tena hadi Jumanne nilipopigiwa simu na Kamanda (wa Polisi) ambaye alinijulisha kuwa mume wangu ameuawa.”
Alisema mume wake amejenga nyumba Kinyerezi ambako wakati mwingine anapokuja Dar es Salaam huenda kukaa huko.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, aliiambia Nipashe jana kuwa wahusika na mauji hayo ni vibaka.
Alisema vibaka hao hawakuwa na bunduki zaidi ya mapanga waliyokuwa wamebeba, ambayo waliyatumia kumshambulia nayo ofisa huyo maeneo ya kichwani.
Sirro alisema vibaka hao walimvamia na kumtaka awape fedha lakini aliwajibu hana ndipo wakaanza kumshambulia.
Alisema walimnyang’anya simu zake mbili za mkononi katika shambulizi hilo la mapanga hadi kukutwa na mauti.
“Hili tukio lilifanywa na vibaka wala hawakuwa majambazi na walimvamia na kuanza kumshambulia na mapanga kichwani lakini ni baada ya kumuomba hela na yeye hakuwa nazo, pia walichukua simu zake mbili,”alisema Kamanda Sirro.
Alisema wanawashikilia watuhumiwa kadhaa kuhusiana na tukio hilo na kwamba wanaendelea kuwasaka wengine waliohusika.
“Hatuwezi kutaja idadi yao kwa sababu upelelezi bado unaendelea wa kuwasaka wote waliohusika na tukio hilo,” alisema Kamanda Sirro.
WAMETEKA WALINZI
Ingawa Kamanda Sirro amedai Malenge aliuawa na vibaka, habari za kuaminika kutoka Kinyerezi juzi zilisema marehemu ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya (OC­CID) ya Kibaha kabla ya kuhamishiwa Uvinza, alikutana na watu ambao walikuwa wamewateka walinzi wa nyumba yake iliyoko Kinyerezi wakati akirudi kutoka katika matembezi.
“Taarifa za awali tulizopata ni kwamba alikuwa anatoka kula maana pale anapoishi haishi na mke,” alisema mmoja wa mtu aliyewahi kufanya kazi na marehemu.
“Ndipo alipokuwa anarudi akawakuta walinzi wake wametekwa nje karibu na nyumbani kwake, akasimamisha gari na kushusha kioo na kuuliza kulikoni.
“Wakati anauliza wale watu walimvamia katika gari lake na kumpiga kichwani na kitu kizito ambapo alifariki papo hapo.”
Aidha, Kamanda Sirro, alisema wanamtafuta Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kinyerezi kwa ajili ya mahojiano, aeleze kwanini kwenye mtaa wake hakuna vikundi vya ulinzi shirikishi.
Alisema alishaagiza maeneo ambako mitaa haijajengeka na hakuna watu wengi, kunatakiwa kuwa na vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuimarisha ulinzi.
“Mtaa ambako ameuliwa huyu Ofisa wetu hakuna watu wengi ni maeneo ya ndani ndani, kulitakiwa kuwe na vikundi vya ulinzi shirikishi kwa ajili ya kulinda usalama wao lakini hakuna hivyo nimemuita Mwenyekiti wa ule mtaa aje ofisini atuambie kwanini kwenye mtaa wake hakuna ulinzi shirikishi,” alisema.
Imeandikwa na Romana Mallya na Mary Geofrey.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MKE WA MKUU WA POLISI WA WILAYA (OCD) ALIYEUAWA AELEZEA UTATA WA KIFO CHA MUMEWE
MKE WA MKUU WA POLISI WA WILAYA (OCD) ALIYEUAWA AELEZEA UTATA WA KIFO CHA MUMEWE
https://1.bp.blogspot.com/-_yWMaQR0P9E/WR3mDsyCKkI/AAAAAAAAbbo/GlLsonnH7WQu6N3p19uLfTNFldTHQ76iQCLcB/s1600/xKamishna-Simon-Sirro-750x375.jpg.pagespeed.ic.M4QKlabXvB.webp
https://1.bp.blogspot.com/-_yWMaQR0P9E/WR3mDsyCKkI/AAAAAAAAbbo/GlLsonnH7WQu6N3p19uLfTNFldTHQ76iQCLcB/s72-c/xKamishna-Simon-Sirro-750x375.jpg.pagespeed.ic.M4QKlabXvB.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/mke-wa-mkuu-wa-polisi-wa-wilaya-ocd.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/mke-wa-mkuu-wa-polisi-wa-wilaya-ocd.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy