MKURUGENZI ALIYETUMBULIWA NA RAIS MAGUFULI AGEUKIA KUHUBIRI INJILI

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandishi Felschemi Mramba amegeukia kuwa mhubiri wa injili baada ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wake.
Uteuzi wa Mramba ulitenguliwa na Rais Dkt Magufuli mapema Januari Mosi mwaka huu baada ya shirika hilo kuwasilisha maombi ya kupandisha bei ya umeme ambapo nafasi yake ilijazwa na Dkt Titto Mwinuka anayekaimu.
Katika kipeperushi kilichokuwa kikisambaa kipitia mitandao ya kijamii, kinaeleza kuwa Mramba atashiriki kwa kufundisha katika semina maalum ya Karama za Roho Mtakatifu na Utendaji wa Nguvu Kuu za Mungu iliyoandaliwa na Kanisa la TAG Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Kipeperushi hicho kinaeleza zaidi kuwa Mramba ataanza semina hiyo kuanzia Mei 30 hadi Juni 4 mwaka huu kuanzia saa 10:30 jioni katika kanisa hilo lililopo Changanyikeni.
FB_IMG_1495820369166.jpg
Mramba alisema kuwa amekuwa akifanya semina hizi kwa muda mrefu sana lakini kipindi cha nyuma hakuwa na muda wa kutosha kama ilivyosasa.
Mramba alifafanua kuwa yeye hajasomea uinjilisti wala uchungaji lakini anapolisoma neno la Mungu na kulielewa hupenda kuwafundisha waumini wengine.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post