MKUU WA POLISI WA WILAYA (OCD) AUAWA NYUMBANI KWAKE TABATA

Mkuu wa Polisi wa wilaya (OCD) ya Uvinza, mkoani Kigoma ameuawa na watu wasiojilikana nje ya nyumba yake Tabata Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Mkuu huyo wa polisi, imeelezwa, alikuwa likizo jijini akitokea Kigoma na alipatwa na umauti saa tatu usiku juzi, baada ya kupigwa na kitu kizito na watu wasiojulikana, alipokuwa anatoka katika matembezi.
Habari za kuaminika zinasema Malenge ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya (OC-CID) ya Kibaha kabla yakuhamishiwa Uvinza, alikutana na watu ambao walikuwa wamewateka walinzi wa nyumba yake iliyoko Kinyerezi wakati akirudi kutoka katika matembezi, ambao walimuua.
“Taarifa za awali tulizopata ni kwamba alikuwa anatoka kula maana pale anapoishi haishi na mke,” alisema mmoja wa mtu aliyewahi kufanya kazi na marehemu.
“Ndipo alipokuwa anarudi akawakuta walinzi wake wametekwa nje karibu na nyumbani kwake, akasimamisha gari na kushusha kioo na kuuliza kulikoni.
“Wakati anauliza wale watu walimvamia katika gari lake na kumpiga kichwani na kitu kizito ambapo alifariki papo hapo.”
Mmoja wa majeruhi ambaye ni jirani wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Urio, alisema juzi majira ya saa 5 usiku akiwa amelala aliamshwa na mlinzi wa nyumba iliyo jirani na marehemu akimtaarifu kuwa wamevamiwa.
Alisema baada ya kuchungulia dirishani aliona gari la marehemu likiwa jirani na nyumba yake na ndipo alipotoka nje kutaka kujua kinachoendelea.
Alisema alipotoka hakumwona mlinzi aliyemuita, lakini alikutana na kijana mwingine mrefu asiyemfahamu ambaye alikuwa ameshika shoka.
Alisema kijana huyo alianza kumshambulia kwa shoka na kumjeruhi eneo la kisogoni.
“Nilijitetea kwa kumwambia jirani yangu (marehemu) nimetoka kukusaidia halafu vijana wako wananipiga,” alisema lakini “kabla sijaendelea kuongea nikajikuta nimepigwa na nondo shingoni na kudondoka chini.”
“Ndipo nikatambaa mpaka nyuma ya choo kwenye kichaka, nilikaa kwa zaidi ya dakika kadhaa ndipo nikainuka na kukimbilia ndani kwangu.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post