MLIPUKO WATIKISA JIJI LA KABUL NA KUUWA WATU WAPATAO 60

Mlipuko mkubwa uliotokea karibu na eneo la majengo ya ubalozi na karibu na makazi ya rais umetikisa Jiji la Kabul nchini Afghanistan.

Maafisa wa Afghanistan wamesema kuwa karibu watu 60 wamepoteza maisha ama kujeruhiwa kwa mlipuko huo hata hivyo wataalam wanaamini idadi inaweza kuongezeka.

Taarifa za awali zinasema mlipuko huo umetokea kwenye gari katika eneo la Zanbaq ambapo nyumba zilizokuwapo umbali wa mita 100 zimeharibika.

Picha za kwenye mitandao ya jamii zinaonyesha moshi mkubwa ukitanda juu ya Jiji la Kabul na magari kadhaa yakiwa yameharibiwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post