MMILIKI WA SHULE YA LUCKY VICENT AFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUSOMEWA MASHTAKA MATANO

Mmiliki na Makamu Mkuu wa Shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha ambayo wanafunzi wake 32 walifariki dunia katika ajali ya gari, wamefikishwa mahakamani leo na kusomewa mashtaka matano yanayowakabili.
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha lilikuwa likimshikilia mmiliki wa shule hiyo, Innocent Mosha kwa tuhuma za kuruhusu idadi kubwa ya wanafunzi na walimu kupanda kwenye gari lake na kupelekea vifo vya watu 35 kati ya 38 waliokuwa katika basi hilo. Jeshi hilo lilisema kuwa basi lilikokuwa limebeba wanafunzi wa Lucky Vicent likielekea karatu kwa ajili ya mtihani wa ujirani mwema lilitakiwa kuwa na abiria 30 tu kwani ndio uwezo wake.
Waliofariki katika ajali hiyo ni wanafunzi 32, walimu 2 na dereva mmoja baada ya gari hilo kupinduka katika eneo la Rotya Wilayani Karatu Jumamosi iliyopita majira ya saa tatu asubuhi.
Makamu Mkuu wa shule hiyo, Logino Vicent hadi jana alithibitisha kuwa mmiliki wa shule alikuwa akishikiliwa na polisi kwa siku ya nne mfululizo kwa ajili ya mahojiano na upelelezi ukiendelea.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post