MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE 19 KUJERUHIWA KATIKA AJALI MAREKANI

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 19 kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari eneo la Times Square mjini New York, Marekani.
Gari hilo linaripotiwa kuacha njia yake na kuingia eneo la watembea kwa miguu katika mtaa wa 45 wa eneo maarufu sana kwa utalii.
Picha zilionyesha gari nyekundu aina ya Honda likiwa limepinduka huku likifuja moshi
Kwa mujibu wa idara ya polisi ya mji wa New York, Dereva wa gari hilo amekamatwa na eneo hilo kufungwa kwa muda.
Dereva huyo kijana mwenye umri wa miaka 26 anaendelea kushikiliwa na polisi huku wakimfanyia uchunguzi kama alitumia kilevi chochote kabla hajaendesha gari hilo. Wengi wamedai kuwa kijana huyo ana historia ya kutumia vilevi.
Polisi waliarifu kuwa gari hilo aina ya Honda lilipoteza muelekeo na kusababisaha ajali hiyo.
Aidha wameongeza kuwa ajali hiyo haijahusishwa na tukio lolote la kigaidi.
Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakiondolewa eneo hilo.
Polisi wanasema kuwa dereva alipoteza mwelekeo na huenda kisa hicho kinaonekana kuwa ajali.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post