MWANACHUO UDOM AKAMATWA NA MISOKOTO 826 YA BANGI

Jeshi la polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu wawili kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi akiwamo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) Nelson Matee mwenye umri wa miaka 24.
Nelson Matee ni mwanafunzi wa kozi ya uuguzi mwaka wa nne katika chuo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kuwa mwanafunzi huyo alikamatwa Mei 9 mwaka huu kufuatia msako mkali uliofanywa na jeshi hilo chuoni hapo ambapo mtuhumiwa alikutwa na jumla ya misokoto 826 ya bangi yenye uzito wa kilo 2.8 akiwa ameiweka kwenye mifuko ya nailoni chumbani kwake.
Kamanda Mambosasa amesema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alisema kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo ya kuuza bangi kwa kipindi cha miaka minne tangu alipojiunga na chuo hicho na kwamba alikuwa akiwauzia wanafunzi wenzake.
Watuhumiwa hao bado wanashikiliwa na polisi na watachukuliwa hatua nyingine za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post