MWANAMKE AMKATA UUME MWANAUME ALIYEMBAKA

Mwanamke mmoja nchini India amezikata sehemu ‘nyeti’ za mwalimu wa dini katika jimbo la kusini la Keral kwa kudai kuwa alimbaka kwa miaka mingi.
Polisi wamesema kuwa mtuhumiwa anayejulikana kama Gangeshananda Theerthapada alikuwa akimtembelea mwanamke huyo katika nyumba yake ili kumfanyia matambiko ya ibada baba wa mwanamke huyo aliyekuwa mgonjwa.
Mama yake alikuwa na matumaini kuwa mtuhumiwa huyo aliyejidai kuwa mtakatifu ataiondolea familia hiyo matatizo. Badala yake alikuwa akimbaka msichana huyo mwenye miaka 23 kila anapotembea nyumba hiyo.
Ijumaa iliyopita mwanamke huyo alichukua kisu na kumshambulia mtuhumiwa alipojaribu kumbaka na baadaye akaita maofisa wa polisi. Mbakaji huyo alikimbizwa hospitalini ili kufanyiwa upasuaji wa dharura kutokana na majeraha aliyoyapata katika ‘nyeti’ zake.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post