MWANAMUZIKI ALIKIBA AMTUNISHIA MSULI DIAMOND PLATNUMZ

Baadhi ya watu huamini kuwa bifu katika muziki zinasaidia muziki kukua na kuchangamka pale tu wasanii na mashabiki wa muziki wakizitumia bifu hizo kwa njia chanya kama vile kununua kazi za msanii wao pendwa, kuhudhuria matamasha, na kumuunga mkono katika mambo mbalimbali anayofanya. Lakini kama bifu itakuwa ni ya maneno matupu, huwakatisha tamaa wasanii na kuwafanya warudi nyuma.
Katika muziki wa Tanzania kwa sasa kumekuwa na watu wawili ambao unaweza kuwaita kama watani wa jadi. Hapa namzungumzia wanamuziki, Alikiba na Diamond Platnumz ambao wote na kila mmoja kwa uwezo wake anafanya vizuri nje na ndani ya nchi.
Kwa hali ilivyo kwa sasa, mashabiki  wa Alikiba wanaona kama vile mwanamuziki huyo amemtunishia msuli Diamond Platnumz baada ya kutangaza kuwa karibuni atazindua biadhaa zake mbalimbali ikiwa ni uwekezaji mkubwa atakaoufanya.
Kauli hii ya Alikiba imekuja ikiwa ni takribani wiki chache tangu mshindani wake katika muziki, Diamond Platnumz alipozindua manukato yake ya CHIBU (CHIBU Perfume) ambayo yanapatikana nchini kwa gharama ya TZS 105,000/=
Alikiba akiwa katika kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds Fm leo Mei 11, 2017 amesema kuwa atazindua mavazi yake (Jeans, Viatu na Tshirts) vyenye jina lake, lakini kama hiyo haitoshi atazindua pia kinywaji cha kuongeza nguvu (Energy drink) yake.
Hii ni hatua kubwa katika muziki wa Tanzania, kwani wasanii sasa wanawekeza ili kuweza kupata kipato hata baada ya wao kuacha kuimba, isiwe kama wasanii wengi wa zamani waliokuwa na majina makubwa lakini baada ya kutoka kwenye muziki maisha yao yakawa ya tabu kutokana na kutowekeza.
Kazi kubwa sasa imebaki kwa mashabiki na watanzania kwa ujumla kuwaunga mkono wasanii ili kukuza tasnia ya muziki nje na ndani ya nchi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post