MWANAMUZIKI DIAMOND PLATNUMZ ADAIWA MILIONI 400

Mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia ameliambia Bunge kuwa mwanamuziki Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz anadaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zaidi ya TZS 400 milioni.
Mbunge huyo aliyasema hayo mjini Dodoma jana wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Mbunge huyo alisema kuwa Wilaya ya Kinondoni kwa sasa ina wasanii wengi na wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi kutokana na mauzo ya kazi zao.
Mtuliwa alisema kuwa mwanamuziki, Diamond Platnumz amemwambia kuwa, kwa sasa anadaiwa na TRA kodi ya zaidi ya TZS 400 milioni.
Kutokana na wasanii hao kuiingizia serikali fedha nyingi kutokana na kazi zao, Mbunge huyo aliomba pia serikali ijikite zaidi katika kuhakikisha ulinzi wa kazi hizo badala ya kutilia mkazo kwenye ukusanyaji wa mapato pekee.
Alipotafutwa kuzungumzia sakata hilo, Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo alisema kuwa suala hilo lipo katika hatua za uchunguzi na hivyo hawezi kulizungumzia.
Chanzo: Nipashe
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post