MWASITI : HUU NI MUDA WA KAZI SIO MAJUNGU

Msanii mkongwe wa muziki, Mwasiti Almas, amedai huu ni wakati wake wa kushirikiana vizuri na management yake mpya ili kuhakikisha anafanya mambo makubwa katika muziki wake.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kaa Nao’, ameiambia Bongo5 kuwa muda mchache aliokaa na management yake hiyo amegundua anaweza kufanya mambo makubwa katika muziki wake tofauti na zamani.
“Kwanza namshukuru Mungu project yetu ya kwanza imeenza vizuri, nimepokea komenti nyingi nzuri, imenifanya niona ni dalili nzuri katika muziki wangu pamoja na management yangu mpya,” alisema Mwasiti.
Aliongeza,”Kwahiyo muda huu kwetu ni kazi juu ya kazi, no majungu. Pia tunajipanga kuachia kazi mpya mwezi Juni. Kaa Nao tayari imeshafanya mambo makubwa sana. Sina mengi zaidi ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano waliotuonyesha, sitawaangusha, huu ni muda wetu wa kazi tu,”
Muimbaji huyo ni mmoja kati ya waimbaji wa kike wa Bongo waliokaa kwenye game ya muziki kwa muda mrefu bila kupotea.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post