NAMNA YA KUMJENGEA MTOTO MAZINGIRA MAZURI YA KUJIFUNZA NYUMBANI

SHARE:

Utakubaliana nasi kuwa shule ya kwanza katika maisha ya mtoto ni nyumbani – wazazi, ndugu wa familia, majirani na marafiki wa familia hus...

Utakubaliana nasi kuwa shule ya kwanza katika maisha ya mtoto ni nyumbani – wazazi, ndugu wa familia, majirani na marafiki wa familia husika. Jukumu la malezi linatoka kwa Mungu na mzazi hana budi kulitekeleza maadam ameamua kumleta mtoto duniani. Kupitia mzazi/mlezi mtoto anapata nyenzo zitakazoongoza maisha yake yote – heshima, utii, unyenyekevu na nidhamu. Yaani wema au ubaya wa mtu mara nyingi ni matokeo ya aliyojifunza nyumbani.
Nyumbani ndiko msingi hujengwa. Bahati mbaya ‘ualimu’ wa nyumbani unatokana na matendo zaidi ya maneno. Mtoto uko naye kila uchao hivyo badala ya kutumia muda mwingi kutoa ‘maelekezo ya tabia njema’. Ishi kwa mfano. Unamwambia mtoto sala na ibada ni muhimu katika maisha – wewe unasali? Je, mnahudhuria ibada pamoja? Kupitia maisha unayoishi utamjengea mtoto misingi ya kiakili na kiimani ili kama ilivyo kwa chakula bora awe na uwiano sawia katika maisha. Bahati mbaya wazazi/walezi wengi huingia katika shughuli hii wakiwa ndiyo kwanza bado vijana. Lugha za ujana na misemo iliyo mingi huwa bado inazo chembe za utovu wa nidhamu. Ukiwa mzazi – mtoto anakusikia, anakuiga. Chagua maneno.
Fursa ya kujenga tabia/kukuza vipaji. Anapotoka tumboni mwa mama, mtoto huwa na kurasa zilizo wazi pasi na tabia za aina iwayo­yote. Isipokuwa kwa vipaji na tabia za kurithi – mzazi/mlezi wewe unalo­jukumu la ‘kuumba’ tabia na kukuza vipaji vya mtoto. Ukiwa kama mwalimu wa kwanza wa mtoto, mwandae kwa ajili ya elimu ya shule (awali, msingi, sekondari, nk.) na stadi za maisha. Muache mtoto ajifunze shughuli tofauti kutoka kwako kulingana na kipaji ulichojaaliwa, shiriki shughuli za jamii ili ajifunze uwajibikaji kutoka kwako.
Umoja wa wazazi/walezi ni wa lazima. Baba na mama wawe wamoja katika kulea. Pale inapotokea tofauti baina yao kuhusu namna ya kutoa maelekezo kwa mtoto – basi na wasibishane mbele ya mtoto. Ikiwa kwa mfano, mama anamwadhibu mtoto na baba hakubaliani na adhabu inayotolewa – muombe mama faraghani na mzungumze juu ya hili. Ukomavu namna hii utasaidia kutomchanganya mtoto na ujumbe unaokinzana. Kamwe msikwaruzane mbele za watoto. Tofauti zenu zivumiliwe mpaka mpatapo faragha mbali na watoto.
Elimu ianze umri gani hasa? Elimu inaanza akiwa tumboni – kupitia mazungumzo ya mama mtoto anaandaliwa kuzijua sauti za watu wake wa karibu kama baba, mashangazi nk. Hii inakwambia kwamba malezi yanaanza mara tu uwapo mjamzito. Punguza ugomvi usio­lazima na ikiwezekana jenga mazingira rafiki kwa kuwa mwenye furaha wakati mwingi. Mara tu unapomtia mikononi mwako kichanga wako – anza kumsemesha. Elimu ya lugha unayotumia ndiyo lugha atakayoanza kuifahamu. Jenga msamiati wenye lugha za staha ili mtoto naye ajifunze hivyo.
Jifunze miongozo ya malezi. Sote tunafahamu kuwa malezi hayana shule eti ukajifunze upate kujua mbivu au mbichi. Nyakati nazo zimebadilika na watu hasa waishio mijini hawakai pamoja na familia tandaa. Hii inamnyima mzazi mpya fursa ya kupata maelekezo ya namna bora ya kulea toka kwa wazazi wazoefu. Pamoja na changamoto hizi, zipo fursa za kujielimisha kupitia vitabu, majarida na makala mfano wa haya. Fursa nyingine adhimu ni mtandao wa intaneti wenye maandiko ya kitaalamu na toka kwa wazazi wa matabaka, makabila na lugha mbalimbali kote ulimwenguni.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: NAMNA YA KUMJENGEA MTOTO MAZINGIRA MAZURI YA KUJIFUNZA NYUMBANI
NAMNA YA KUMJENGEA MTOTO MAZINGIRA MAZURI YA KUJIFUNZA NYUMBANI
https://4.bp.blogspot.com/-GzD_K07ZSmw/WSH19qf7stI/AAAAAAAAbo8/_Ht7wlvpfQwHIQCZYpT7gapKqIR7VEWkwCLcB/s1600/xfather-and-children-reading-750x375.jpg.pagespeed.ic.KJU-2m_bEp.webp
https://4.bp.blogspot.com/-GzD_K07ZSmw/WSH19qf7stI/AAAAAAAAbo8/_Ht7wlvpfQwHIQCZYpT7gapKqIR7VEWkwCLcB/s72-c/xfather-and-children-reading-750x375.jpg.pagespeed.ic.KJU-2m_bEp.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/namna-ya-kumjengea-mtoto-mazingira.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/namna-ya-kumjengea-mtoto-mazingira.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy