NAPE AMJIA JUU MAKONDA KUHUSU UVAMIZI KITUO CHA CLOUDS

Mbunge wa Matama, Nape Moses Nnauye amemjia juu kwa mara nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusema kwamba hakuunda kamati ya kumchunguza yeye, bali aliunda kamati ya kuchunguza tukio la kuvamiwa kwa kituo cha utangazaji cha Clouds Media Group.
Nape ameyasema hayo mapema leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo alieleza kwamba, kama kiongozi huyo alikuwa ni mmoja wa wavamizi wa kituo hicho, basi hayupo juu ya sheria.
“Niliunda kamati kuchunguza tukio la kuvamiwa kituo cha utangazaji sio kumchunguza RC. Kama RC alikuwa mmoja wa wavamizi, hayuko juu ya sheria,” aliandika Nape
Alipoulizwa kwanini Waziri wa Habari aunde kamati ya uchunguzi wa tukio la uvamizi badala ya kamati hiyo kuundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Nape alijibu kwa kuuliza swali kama kila kamati inaundwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
@Nnauye_Nape WAZIRI wa Michezo unaunda tume ya kuchunguza uvamizi, sasa WAZIRI wa Mambo ya Ndani na polisi wafanye kazi gani??
@abdulmandanje Tumia akili usisukumwe na njaa, kila kamati inaundwa na Wizara ya mambo ya ndani? Njaa mbaya dogo

Majibu haya ya Nape yamekuja ikiwa ni saa chache baada ya kuulizwa ni yapi maoni yake kuhusu kauli ya Makonda kwamba hakuwa akifahamu mipaka yake ya kazi ndio sababu alikwenda kuunda tume ya kumchunguza.
@Nnauye_Nape Kaka kwa mujibu wa Makonda ulikuwa hujui mipaka yako ya kazi ndio maana ulikurupuka kuunda tume, tena isio na sifa.nini maoni yako?

Kauli ya Nape kuhusu kuunda kamati imekuja ikiwa ni takribani saa 24 tangu Makonda aliposema kuwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aliunda kamati ya kumchunguza.

Makonda alisema hayo jana, ambapo alidai kuwa kamati iliyoundwa na Waziri isingeweza kumhoji kwa sababu haikuwa na uwezo huo kutokana na wajumbe wa kamati hiyo kutofahamu mambo yanayohusiana na masuala ya uvamizi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post