NICK MINAJ AWALIPIA ADA MASHABIKI WAKE

Msanii wa muziki wa rap nchini Marekani, Nick Minaj amewalipia ada wanafunzi waliofaulu kwa kupata daraja A.
Nick Minaj amekuwa miongoni mwa wasanii wachache walioamua kuipa kipaumbele elimu kwa kuwasaidia wanafunzi nchini Marekani.
Mei 7 mwaka huu Nick Minaj katika ukurasa wake wa Twiter aliandika akisema kuwa wanafunzi waliopata daraja A wamwonyeshe matokeo yao kwa lengo la kukuza video yake mpya aliyoitoa ya ‘Regret In Your Tears’ lakini mambo yalibadilika baada ya mtu mmoja kujibu katika tweet’ yake akimwomba kama anaweza kumlipia ada yake ya shule.

Show me straight A's that I can verify w/ur school and I'll pay it. Who wants to join THAT contest?!?!🤷🏽‍♀️ Dead serious. Shld I set it up? https://twitter.com/cjbydesign/status/861073053312307200 
Ndipo Minaj alipoamua siyo tu kumsaidia kijana huyo, bali na wengine wwaliokuwa wakihitaji msaada wa kulipiwa ada na wenye mikopo ya elimu.
Katika ‘post’ aliyoiweka katika ukurasa wake wa  mtandao wa ‘instagram’, Nick Minaj alielezea furaha aliyo nayo baada ya kuwalipia wanafuzi nane jumla ya dola za kimarekani 18,000 sawa na shilingi za kitanzania milioni 40.2 ikiwa inajumuisha ada, kulipa madeni ya elimu wanayodaiwa pamoja na kununua vitabu.


Nick Minak hakuishia hapo tu, bali alisema kuwa hivi karibuni atafungua kituo cha kuwasaidia wanafunzi wengi zaidi.
Devonte Portis, mwanafunzi anayesomea fani ya Uhusiano wa Umma katika Chuo Kikuu cha Ohio pamoja na rafiki yake Christina Holland ni miongoni mwa walionufaika na msaada huo alioutoa Nick Minaj.
“Imekuwa ni bahati kubwa, ni baraka!, ametulipia mikopo yetu ya elimu. Ndani ya wiki moja amehakikisha kuwa kila kitu kinawekwa sawa na tumeshasajiliwa kuendelea na masomo wakati huu wa majira ya joto,” alisema Portis.
Portis aliongeza kuwa anashukuru na anafurahia kuwa shabiki wa msanii ambaye anawajali mashabiki wake kwa hali na mali.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post