OMMY DIMPOZ YAMEMFIKA HAPAA..AMTAKA MADEE AFANYE JAMBO HILI KWA DOGO JANJA

Kauli ya Dogo janja ya kusema kwamba wasanii wengi wanavaa kikongo imemfanya Ommy Dimpoz kuomba akaguliwe kwanza kama code yake imekaa poa.
Kama ni miongoni mwa mashabiki ambao mlikuwa karibu na mtandao wa kijamii wa Instagram katika kurasa ya Dogo janja najua utakuwa umekutana na vitambo vingi sana vya Janjaro kuhusu uvaaji wake na kufunguka kwamba hakuna anayependeza kama yeye Dar, huku vingine akifunguka kwamba wasanii wengi wanavaa kikongo na kuchangana marangi mengi ambayo yanaweza kumfanya kinyonga kuchanganyikiwa.
Sasa tukiwa bado tunamtazama Dogo janja na staili yake ya mavazi anayotupia, Ommy Dimpoz akaona sio kesi auulize kwanza kwa Dogo janja kama mtupio wake uko onpoint, kupitia kurasa yake Dimpoz aliandika hivi Rais @madeeali muulize @dogojanjatz vipi nimepatia code 😄 maana nasikia yeye ndo king wa code😉
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post