PICHA: MUME WA ZARI ALIVYOFUKIWA NA FEDHA KWENYE KABURI LAKE

Jana jioni mwili wa mfanyabiashara maarufu na mume wa Zarinah Hassan (Zari The Boss Lady) ulizikwa nchini Uganda baada ya kufariki wiki iliyopita nchini Afrika Kusini alipokuwa akiishi.
Watu mbalimbali walihudhuria mazishi hayo kutokana na Ivan Semwanga kuwa alikuwa ni mtu tajiri na aliyefahamika na wengi.
Katika maziko hayo, kilichowashangaza wengi ni jinsi matajiri wenzake walivyoamua kumuenzi mwenzao huyo kwa kumwaga fedha ndani ya kaburi hilo kabla jeneza halijawekwa. Kitendo hicho kiliwashangaza wengi kwa sababu si utamaduni wa kiafrika kwani itaonekana kana kwamba mnasherehekea kifo chake jambo ambalo ni mwiko.
No automatic alt text available.Mbali na tukio hilo, watoto wa marehemu, Ivan Semwanga walionyesha masikitio yao baada ya kuondokewa na baba yao, ambapo walisema kuwa maisha kwao hayawezi kuwa sawa tena sababu ya pengo hilo.
“Dad, so many thoughts come to our mind whenever we speak of your name; it seems without you in our lives things will never be the same. We think of the good old days when we were still so little; consumed in your love, and in your smile.”
“Those days are gone and no matter what we do, life will never be the same! Oh Dad, if only we could turn back the hands of time and hear your voice once more, but God called you to a better place, so peaceful and free of pain. And when we see you sleeping, we can only wish the best for you.”
Ivan Semwanga alifariki katika Hospitali ya Biko Academy nchini Afrika Kusini, Alhamisi wiki iliyopita kutokana na ugonjwa wa moyo na alizikwa jana Mei 30, 2017 nchini Uganda.
Hapa chini ni picha nyingine za matukio wakati wa mazishi yako;

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post