PICHA: RAIS DKT MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Mei, 2017 amemuapisha Bw. Tixon Tuyangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – anayeshughulikia Elimu.
Viongozi wengine walioapishwa na Mhe.Rais Dkt. Magufuli ni Bwa. Rajab Omar Luhwavi ambaye anakuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji.
Bw. Bernard Mtandi Makali ameapishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa na Bw. Clifford Katondo Tandari, kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro.
Pia Rais Magufuli amemuapisha Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Viongozi wote walioapishwa wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa hali ya juu katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Hafla ya kuapishwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Tixon Tunyangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Rajab Omar Luhwazi kuwa Balozi nchini Msumbiji Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Bernard Mtandi Makandi kuwa katibu Tawala Mkoa wa Rukwa  Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Clifford Katondo Tandari kuwa katibu Tawala Mkoa wa Morogoro  Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)  Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Viongozi walioapishwa wakila kiapo cha maadili ya utumishi wa umma
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Mei, 2017
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post