PICHA: TRENI YA ABIRIA YAPATA AJALI USIKU MKOANI MOROGORO

Treni ya abiria iliyokuwa inakwenda Bara imepata ajali usiku wa kumakia leo majira ya saa 5:25 katika eneo la Stesheni ya Mazimbu mkoani Morogoro. Katika hajali hiyo ilihusisha mabehewa saba ambapo manne yakiwa yameegama na matatu yameacha reli.
Abiria mmoja, Ashura Mrisho aliyekuwa anasafiri kwenda Tabora amepata maumivu baada ya kuangukiwa na mizigo ilikuwamo ndani ya behewa moja.
Mabehewa 13 yamerejeshwa Morogoro kuwapangia usafiri mbadala abiria wa treni hiyo.
Shirika la Reli Tanzania (TRL) linafanya utaratibu wa kuwasafirisha abiria wa bara kwa mabasi hadi Kijiji cha Lukobe Manispaa ya Morogoro ambapo watapanda treni kwenda bara. Kuhusu wale wa treni ya kuja Dar es Salaam kutoka bara ambayo itasimama Lukobe, watasafirishwa kwa mabasi kurudi Morogoro kuendelea na safari.
Taarifa zaidi zitafuata wakati uongozi wa TRL, mafundi na wahandisi wakishughulikia ajali hiyo.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post