POLEPOLE AELEZA RAIS MAGUFULI ALIVYOKATAA WALIOTAKA KUHONGA KUHUSU MCHANGA WA MADINI

Ni siku mbili zimepita sasa tokea nchi iingie kwenye vuguvugu la kupambana na wahujumu uchumi ambao wanadaiwa kulipotezea taifa letu fedha nyingi kutokana na uzembe wa watu wachache.
Siku ya Jumatano Mei, 24 mwaka huu, Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokea ripoti ya kamati aliyoiunda kuchunguza kiwango cha madini kilichopo mchanga wa madini uliokuwa tayari kusafirishwa kwa makontena kwenda nchi za nje kwa ajili ya kuchakatwa.
Rais magufuli akiipokea taarifa hiyo alitoa hotuba yake ambayo ndani yake alieleza kwa uchungu mkubwa namna ambavyo amesikitishwa na vitendo vua uhujumu uchumi vilivyokuwa vinaendelea jambo ambalo lilimfanya atengue uteuzi wa waziri mwenye dhamana ya kusimamia madini, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo pamoja na kuivunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA).
Siku iliyofuata Mei 25, 2017 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole aliibuka na kudai kuwa kuna wahujumu uchumi walitaka kuhonga kiasi cha Bilioni 300 ili kusitisha zoezi la uchunguzi huo, huku akihoji masilahi wanayopata watu wanaofanya biashara ya kusafirisha makinikia hayo nje ya nchi.
“Vita ziko za aina nyingi, ziko zile tunazopigana kwa silaha mtu na mtu, na nchi na nchi, lakini sasa ziko vita za kiuchumi, ni mbaya zaidi zinalenga kuturudisha nyuma.Wahujumu uchumi hawapigani na Rais, bali wanapigana na maisha ya wananchi wa Tanzania, tukiwa wamoja tutashinda vita hii, wako watu wanaipinga vita hii yenye dhamira njema, huu si wakati wa kutofautiana ni wakati wa kusimama kumshinda adui,” alisema Polepole.
Polepole aliendelea kueleza kuwa palikuwapo na watu waliotaka kutoa Tsh bilioni 300 ili kusitishwa kwa zoezi la uchunguzi wa mchanga huo wa madini lakini Rais Dkt Magufuli aliwakatalia.
“Walitaka kuhonga bilioni 300 kwa ajili ya kusitisha uchunguzi huo, hivi wao wanapata fedha kiasi gani? Lakini rais akawatolea nje, akasema subirini uchunguzi ukamilike. Tusimame naye na hakika tutashinda na historia itaandikwa kwamba tulisimama katika kulinda urithi wetu,” amesema.
Kauli hii ya kiongozi wa CCM imezua maswali mengi, huku wengine wakisema kama watu hawao wanadaiwa kutaka kuhonga bilioni 300 ambayo ni fedha ya bajeti ya wizara mbili, je wao huwa wanapata faida kiasi gani?
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post