POLISI WAELEZA CHANZO CHA AJALI ILIYOPELEKEA VIFO VYA WATU 35 MKOANI ARUSHA

SHARE:

Ajali ya basi la Shule ya Lucky Vicent iliyotokea wilayani Karatu na kusababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja vin...

Ajali ya basi la Shule ya Lucky Vicent iliyotokea wilayani Karatu na kusababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja vingeweza kuzuilika au kuwa pungufu kama basi hilo lingekuwa na mikanda na kila mmoja akaufunga kabla ya kuanza safari.
Kamanda wa Polisi Msaidizi wa Mkoa wa Arusha, Yusuf K Ilembo amesema kuwa wengi waliofariki katika ajali ile ni kutokana na kuumia ndani ya mwili kulikosababishwa na kugongana wakati ajali ilipotokea.
“Wangekuwa wamefunga mikanda, huenda vifo vingekuwa vichache au visiwepo kabisa” alisema. Aidha Kamanda Ilembo alisema pia, hata mwendo kasi wa basi hilo ulichangia kupata ajali na kupelekea vifo vya watu 35.
Wwatu 33 walifariki papo hapo, huku mmoja wakati akikimbizwa hospitali na mwingine wakati akipatiwa matibabu.
Kamanda Ilembo alisema kuwa kutokana na ajali iliyotokea Mei 6, mwaka huu Polisi wanalazimika kuyafanyia ukaguzi magari yote yanayotumiwa na shule mbalimbali kuwasafirisha wanafunzi ili kujihakikishia usalama wake.
Alisema kwamba ukaguzi wa awali wa basi dogo lenye namba za usajili T 781 BYS halikuwa na mikanda kama ilivyotakiwa na sheria ya usalama barabarani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alieleza kuwa gari aina ya Mitsubish Rosa lililohusika katika ajali iliyoua watu 35, lilikuwa limebeba abiria 38 wakati uwezo wake ukiwa ni abiria 30 tu.
Katika ajali hiyo waliosalimika ni abiria watatu tu kati ya 38 waliokuwamo ndani ya basi hilo wakati linapata ajali.
“Kwa sasa tutatilia mkazo ukaguzi wa magari yote yanayotumika kusafirisha wanafunzi ili kujua kama yana uwezo na sifa za kutumika kwa shughuli hiyo. Pia maafisa wetu watazitembelea shule mbalimbali zenye magari ya kusafirisha wanafunzi ili kutoa elimu kuhusiana na usalama wa barabarani,” alisema.
Ilembo aliongeza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya uongozi wa shule zitakazobainika kuwa na mabasi yasiyo na ubora na kiwango cha kuwasafirisha wanafunzi.
Alithibitisha kuwa Mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent, Innocent Moshi anashikiliwa na jeshi la Polisi Arusha kwa ajili ya mahojiano.
“Bado yupo mikononi mwa polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na ajali iliyotokea. Tunataka kujua kama basi lile lilikuwa na viwango vya kuwasafirisha wanafunzi,” alisema.
Wakuu wa Shule mbalimbali jijini Arusha wamethibitisha kuwa polisi na maafisa wa usalama barabarani wamefika katika shule zao ili kuyafanyia ukaguzi magari yote yanayotumika kusafirisha wanafunzi katika shule hizo.
Mkuu wa Shule ya Lady of Mercy iliyoko Kimandolu, Irene Mogusu alieleza kuwa siku ya Jumatano maafisa wa usalama barabarani walifika katika shule yake kwa ajili ya ukaguzi.
Inakadiriwa kuwepo kwa shule binafsi za awali, msingi pamoja na sekondari zaidi ya tisini katika mkoa wa Arusha peke yake. Na magari mengu ya shule hizo yana rangi ya njano.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: POLISI WAELEZA CHANZO CHA AJALI ILIYOPELEKEA VIFO VYA WATU 35 MKOANI ARUSHA
POLISI WAELEZA CHANZO CHA AJALI ILIYOPELEKEA VIFO VYA WATU 35 MKOANI ARUSHA
https://4.bp.blogspot.com/-Ba0chMmwnIg/WRODWLOkTnI/AAAAAAAAbEE/NgwG-pmkopkHVHBoQ7nIpmLByhj0TEk4ACLcB/s1600/xWhatsApp-Image-2017-05-06-at-11.28.22-640x375.jpeg.pagespeed.ic.vNwHSQOx0I.webp
https://4.bp.blogspot.com/-Ba0chMmwnIg/WRODWLOkTnI/AAAAAAAAbEE/NgwG-pmkopkHVHBoQ7nIpmLByhj0TEk4ACLcB/s72-c/xWhatsApp-Image-2017-05-06-at-11.28.22-640x375.jpeg.pagespeed.ic.vNwHSQOx0I.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/polisi-waeleza-chanzo-cha-ajali.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/polisi-waeleza-chanzo-cha-ajali.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy