POLISI YAWAKAMATA WATUHUMIWA WA MAUAJI MKOANI PWANI

SHARE:

PWANI:  Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, ambaye pia anakaimu Wilaya ya Kibiti, Juma Njwayo,  amesema vyombo vya dola vimewakamata watu kadhaa wa...

PWANI: Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, ambaye pia anakaimu Wilaya ya Kibiti, Juma Njwayo,  amesema vyombo vya dola vimewakamata watu kadhaa wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu wa wakazi mbalimbali katika maeneo ya Mkoa wa Pwani.
Njwayo alisema kuwa, licha ya watuhumiwa hao kukamatwa lakini bado vyombo vya dola vinaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo.
 “Kuna watu wanaoshukiwa ambao ni wengi wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa, kuna wengine wanatafutwa na wakipatikana watahojiwa, lakini hawajakamatwa kwa maana ya kwamba imethibitika wao ni wahalifu,” alisema.
Mkuu hiyo wa Wilaya hakuwa tarari kutaja idadi ya watuhumiwa waliokamatwa hadi sasa kwa kile alichoeleza kuwa, yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hawezi kutoa siri.
Wakati huo huo, kiongozi huyo aliwataka wananchi wa maeneo hayo kuendelea na shughuli zao za kile siku lakini pia wachukue tahadhari kuhusu usalama wao.
“Watu wanalima, wanaofanya shughuli za Serikali wanafanya, lakini haya yanafanyika tunapata uthibitisho kwa mfano wa hawa watu wanne waliouawa huku Rufiji, kwa hiyo hali iko hivyo. Tunaomba watu sasa wafanye shughuli zao kwa tahadhari, wakiona mtu wasiyemjua watoe taarifa katika vyombo.
“Pia kama wanazo taarifa watuambie, sisi tunajua hawa watu wako kwenye jamii, haiwezekani mtu asiyekujua wewe aje akupige risasi jioni, lazima awe anakujua na kama hakujui basi anashirikiana na mtu anayekujua. Hivyo tunawasisitiza hawa wananchi wetu wawe na tahadhari ya kiusalama,” alisema.
Alipoulizwa amebaini nini katika matukio hayo yanayowalenga zaidi viongozi wa Serikali, alisema suala hilo ni gumu na bado haijajulikana sababu ya uhalifu huo.
“Hatujui sababu ni nini, lakini ni kweli watu wote waliopata hilo tatizo wapo askari, wapo viongozi ama ni wa serikali ya vijiji au chama tawala,” alisema.
Awali, Njwayo alikiri wazi kuwa wananchi katika maeneo hayo wanaishi kwa hofu kwa sababu matukio si ya kawaida.
“Lazima uhofu, yaani upo nyumbani kwako unakula mtu anakuja anakupiga risasi, watu nao wanasikia mlio wa risasi lazima wapate hofu, hilo ni jambo la kila mtu mwenye akili yake timamu lazima ahofie.
“Lakini sisi kwa upande wetu wa wilaya halitupendezi jambo hili, tuna hatua nyingi tunazichukua kwa kushirikiana na Serikali Kuu kupambana na jambo hili,” alisema.
Kauli ya Njwayo imekuja siku chache baada ya watu wasiofahamika kumuua Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Muyui, Iddy Kirungi, huku mtoto wake, Nurdin Kirungi, akipigwa risasi ya tumbo wilayani Kibiti.
Wauaji hao baada ya kutekeleza unyama huo walitokomea kusikojulikana, hali inayotishia usalama wa raia na mali zao, huku wengine wakilazimika kuzikimbia nyumba zao kwa hofu ya kupoteza maisha.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema linaendelea kuwasaka wahalifu na kuimarisha ulinzi.
Katika toleo la jana, gazeti hili lilimkariri, Diwani wa Kata ya Mtunda, Omary Twanga (CCM), akisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 17, mwaka huu saa 1:30 usiku na Kirungi aliuawa akiwa nyumbani kwake.
Tukio hilo ni mwendelezo wa matukio ya mauaji ya watu mbalimbali, wakiwamo askari wa Jeshi la Polisi, viongozi wa vyama na Serikali za vijiji mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa rekodi za matukio ya mauaji katika mkoa huo, ni kwamba hadi sasa zaidi ya watu 30 wameuawa.
Tukio la hivi karibuni ni lile lililotokea Mei 13, mwaka huu, ambapo Katibu wa CCM Kata ya Bungu, Wilaya ya Kibiti, Halife Mtulia, kupigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana alipokuwa akitoka uani.
Aprili 14, mwaka huu, askari nane waliuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika Kijiji cha Makengeni, wilayani Kibiti.
Pia Januari 19, mwaka huu, Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Nyambunda, Oswald Mrope, aliuawa baada ya kupigwa risasi mbele ya familia yake na Februari 3, mwaka huu watu wasiojulikana walivamia nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Jaribu, Bakari Msanga, wakaichoma moto, huku yeye mwenyewe akifanikiwa kuwatoroka.
Februari, mwaka huu, watu watatu, akiwamo Ofisa Upelelezi wa Wilaya (OC CID) ya Kibiti mkoani Pwani, Mrakibu wa Polisi, Peter Kubezya, waliuawa kwa risasi.
Machi Mosi, mwaka huu, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambunda, Said Mbwana, naye aliuawa.
Aprili 29, mwaka huu, mkazi wa Kijiji cha Mgomba Kaskazini, Kata ya Mgomba, Ikwiriri, Hamad Malinda, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Mei 5, mwaka huu, Kada wa CCM Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, Amir Chanjale, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Oktoba 24, mwaka jana, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyambunda, Ally Milandu, alipigwa risasi na kufariki dunia na Novemba 6, mwaka jana, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyang’unda, Kijiji cha Nyambunda, Mohammed Thabiti, alipigwa risasi akielekea kwake.
Wengine waliouawa ni Ofisa wa Misitu aliyekuwa Mkaguzi wa Kituo cha Ukusanyaji Mapato ya Ushuru katika Kijiji cha Jaribu, Peter Kitundu na Rashid Mgamba, ambaye ni mlinzi na mgambo walipigwa risasi kichwani na begani na walifariki dunia papo hapo eneo la tukio.
Pia Katibu wa CCM Wilaya ya Kibiti, Zena Mgaya, alikaririwa na vyombo vya habari akisema Kijiji cha Nyambunda, Kata ya Bungu, kimeshapoteza mwenyekiti, mtendaji na wenyeviti watatu wa vitongoji vilivyoko katika kijiji hicho.
MTANZANIA.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: POLISI YAWAKAMATA WATUHUMIWA WA MAUAJI MKOANI PWANI
POLISI YAWAKAMATA WATUHUMIWA WA MAUAJI MKOANI PWANI
https://1.bp.blogspot.com/-fLYwwai_XqQ/WR_4XtiKfMI/AAAAAAAAblo/EVLo3ObLUJQMqchsz6FosdXV2r0phVd0QCLcB/s1600/xDSC02454-750x375.jpg.pagespeed.ic_.pJju1JcDaM.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-fLYwwai_XqQ/WR_4XtiKfMI/AAAAAAAAblo/EVLo3ObLUJQMqchsz6FosdXV2r0phVd0QCLcB/s72-c/xDSC02454-750x375.jpg.pagespeed.ic_.pJju1JcDaM.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/polisi-yawakamata-watuhumiwa-wa-mauaji.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/polisi-yawakamata-watuhumiwa-wa-mauaji.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy