RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA TBC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ziara ya kushtukiza katika makao makuu ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) yaliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa ambaye hakutaka jina lake kutajwa alieleza kuwa, Rais Magufuli aliwasili kituoni hapo majira ya saa 5 asubuhi, na miongoni mwa mambo aliyoyafanya ni kusikiliza changamoto zinazowakumba wafanyakazi wa shirika hilo.
“Rais alitembelea hapa majira ya asubuhi na alizungumza na wafanyakazi wa TBC. Ujio wake ulikuwa ni kwa lengo la kujua hasa changamoto tunazokabiliana nazo katika eneo letu la kazi,” kilisema chanzo hicho.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post