RAIS MAGUFULI AWAHAKIKISHIA MAZINGIRA SALAMA WAWEKEZAJI KUTOKA AFRIKA KUSINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wafanyabiashara na wawekezaji wa Afrika Kusini kujitokeza na kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ina mazingira yaliyo salama, bora na fursa wezeshi.
Rais Magufuli aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini katika mkutano wa wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliojadili fursa na vivutio vya uwekezaji katika mataifa hayo.
Rais Magufuli alisema Tanzania ina vivutio mbalimbali vya uwekezaji vyenye kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Afrika Kusini kuwekeza katika sekta yoyote nchini kwani uwekezaji huo una uhakika wa kuzaa matunda mazuri.
“Napenda kuwahakikishia wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza Tanzania kuwa nchi hii ina amani tangu tupate uhuru mnamo mwaka 1961,ina mazingira mazuri ya kibiashara,utulivu wa kiasiasa pamoja na uchumi unaotabirika hivyo nawasihi wafanyabiashara wa Afrika Kusini kuwekeza nchini kwetu,” alisema Dkt. Magufuli.
Aliongeza kuwa Tanzania ina soko kubwa la kuuzia bidhaa na kutoa huduma mbalimbali kwani tumezungukwa na nchi nane ikiwemo ya Burundi, Congo, Malawi, Rwanda, Uganda na Zambia, na kwa kiasi kikubwa zinashirikiana na Tanzania katika kufanya biashara za kimataifa hivyo wakiwekeza Tanzania watapata soko la nchi nyingi.
Kwa upande wake Rais wa Afrika Kusini. Jacob Zuma alisema kuwa wamekubaliana na Rais Magufuli kukuza ushirikiano hasa wa kiuchumi wa nchi zote mbili ikiwa ni moja ya kichocheo kitakachosaidia kuleta faida na kutunza ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya nchi hizo mbili.
“Hadi sasa kuna zaidi ya Makampuni 200,000 kutoka Afrika Kusini ambayo yamewekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo, mawasiliano, sekta za fedha, ujenzi, madini na utalii lakini kwa kuwa Tanzania ina mazingira mazuri ya kuwezesha ukuaji wa uchumi tunaamini kampuni hizo zitaongezeka,” alisema Rais Zuma.
Vile vile alitoa rai kwa nchi hizo mbili kuacha kujikita katika bidhaa pekee kwani sio endelevu na haitengenezi ajira za uhakika na badala yake kuwekeza nguvu katika uzalishaji.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post