RAIS MAGUFULI NA RAIS ZUMA WA AFRIKA KUSINI KUBADILISHANA WALIMU

Serikali ya Tanzania na Afrika kusini zitasaini mikataba mbalimbali ikiwemo ya elimu itakayotoa fursa ya kubadilishana walimu.
Mikataba hiyo itasainiwa kesho baada ya kuwasili kwa Raid wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, atakayefanya ziara ya siku tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Agustine Mahiga, alisema ujio wa Rais huyo utatoa fursa ya kujadili zaidi juu ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya nchi hizo.
Alisema Rais Zuma ataongozana na mawaziri wake sita na wafanyabiashara 80, jambo litakalotoa fursa ya kukuza uhusiano wa kibiashara.
“Ziara hii inafanyika baada ya Rais Magufuli kumualika Zuma wakati walipokutana mjini Addis Ababa, Ethiopia kwenye mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika (AU), Hakika ujio huu utakuwa na manufaa makubwa kwetu,” alisema.
Alisema kiwango cha biashara kinachofanywa na Afrika Kusini hapa nchini kwa sasa kimeongezeka hadi kufikia dola za kimarekani bilioni 2.2 kwa mwaka 2016 kutoka dola za kimarekani milioni 900.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post