RAIS ZUMA AONDOKA KWA HASIRA KWENYE MKUTANO WA MEI MOSI BAADA YA KUZOMEWA

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameondoka katika mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) baada ya kuzomewa na wafanyakazi wakishinikiza ajiuzulu urais.

Ngumi pia zimetokea katika mkutano huo baina ya wafuasi wanaomuunga mkono rais Zuma na wapinzani wake jambo lililopelekea hotuba zote zilizopangwa kutolewa kwa ajili ya Mei Mosi kutotolewa.

Shirikisho la Wafanyakazi nchini humo COSATU, lilitoa wito mwezi uliopita wa kumtaka rais Jacob Zuma kuachia madaraka baada ya kumfukuza kazi waziri wa fedha anayekubalika mno.


Licha ya kuwepo kwa shinikizo la kumtaka kujiuzulu rais Zuma ameapa kubakia madarakani hadi hapo muhula wake utakapomalizika mwaka 2019.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post