RAY C AWAFARIJI MAJERUHI WA AJALI YA BASI KARATU

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila, maarufu kama Ray C ametumia vizuri siku ya leo ya akina Mama Duniani kwa kuwakumbuka wazazi wa watoto watatu walionusurika kwenye ajali ya basi huko Karatu mkoani Arusha kwa kuwapa ujumbe wa faraja wenye maneno ya kutia Moyo.
Ray C amesema Mungu yupo mbele ya watoto hao na kwa vile wameondoka wakiwa wanahema basi watarudi wakiwa wanahema na wenye Afya.
Mtapona kwa nguvu ya Mungu kupitia madaktari….na mtarudi salama…Ya Mungu ni mengi na tayari kashawaonyesha kupitia mliyopitia na bado mnahema” Ameandika Ray C .
Ray C pia aliwapa moyo akina mama wa watoto hao watatu ukizingatia leo ni siku ya Akina Mama duniani kwa kusema waendelee kuomba na kumuamini Mungu kwani yeye ndiye ngao pekee iliyobakia kwenye maisha yao.
Happy Mother’s day kwa wamama wote Wa hawa watoto,Mungu azidi kuwaonyesha uwepo wake kwenu muda wote na mzidi kumuamini kuwa yeye ndio ngao ya Maisha yenu” Ameandika Ray C kwenye ukurasa wake wa Instagram.


Watoto hao watatu majeruhi wa ajali ya Basi ya Karatu iliyoua watu 35 pamoja na wazazi wao, wameondoka leo asubuhi hapa nchini kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya Matibabu zaidi .
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post