RC ARUSHA ATOA UFAFANUZI WA MATUMIZI YA RAMBIRAMBI LUCKY VICENT

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAPATO NA MATUMIZI YA MSIBA WA
AJALI YA LUCKY VICENT MKOANI ARUSHA
TAREHE 21 MAY 2017
Mnamo tarehe 19 May 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha ilitoa taarifa ya mapato na matumizi kuhusu michango ya Rambirambi ya ajali ya basi ya shule ya Lucky Vincent iliyotokea Wilayani Karatu eneo la Rhotia. Ajali hiyo ilitupotezea wapendwa wetu 35, wakiwemo wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1.
Aidha ajali hiyo ilitubakishia Majeruhi 3 ambao hali zao zilikuwa ni mbaya sana. Tunaamini Mwenyezi Mungu ana makusudio yake kuwaacha hai hawa majeruhi 3 kwenye ajali mbaya kama ile.
Baada ya Serikali na wadau mbalimbali nchini kushirikiana kufanikisha kuhifadhi miili ya wapendwa wetu ikiwa ni pamoja na kutoa fedha taslimu za rambirambi kiasi cha shilingi 3,857,000 kwa kila familia iliyofiwa kwa familia zote 35. Kwa ujumla tumeona ni vyema sasa nguvu kubwa ikapelekwa kwenye kuwahudumia majeruhi ili waweze kupona na makusudio ya Mungu yaweze kutimia.
Tunapenda kuujulisha Umma kuwa hadi Ijumaa ya tarehe 20 May 2017 kutokana na wadau kuendelea kuchangia tumebakiwa na kiasi cha shilingi 67,993,885. Kwa mantiki hiyo busara imeelekeza kuwa nguvu kubwa saa ipelekwe kwenye kuwahudumia majeruhi, maana hata tufanyeje kwa wale ambao Mungu kwa mapenzi yake amewachukua hatuna namna tena ya kuwarudisha.
Hivyo tunapenda kuujulisha Umma kuwa Jumatatu tarehe 22 May 2017 tutazitumia familia za majeruhi pamoja na madaktari wetu waliojitoa kuwasindikiza majeruhi kiasi cha Dola za kimarekani 20,000 (Sawa na44,720,000 kwa Exchange rate ya 2,236) kila familia itapata Dola 5,000 (Jumla ni Dola 15,000 kwa familia 3), Daktari Dola 2,500 na muuguzi Dola 2,500 kama sehemu ya kuendelea kuwafariji na kuwapunguzia changamoto huko ugenini.
Kwa ujumla baada ya yote hayo tutabakiwa na kiasi cha shilingi 23,273,885 huku tukiendelea kuangalia hali za majeruhi wetu. Kiasi cha fedha kilichobaki kitaendelea kuwekewa utaratibu kupitia timu ya wafiwa 4 walioteuliwa na wafiwa wenzao kushirikiana na Serikali kuhakikisha mapato na matumizi ya suala hili yanaeleweka vyema kwa Umma.
Pia tunapenda kuuhabarisha Umma kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha imehitimisha rasmi zoezi zima la kupokea rambi rambi ili ipate muda zaidi wa kufuatilia Mustakabali wa Majeruhi wetu walioko hospitalini nchini Marekani.
Imetolewa na:
Mrisho Mashaka Gambo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post