REAL MADRID YAICHAKAZA GRANADA NA KUFUNGANA POINTI BARCELONA

Timu ya Real Madrid imefikisha pointi sawa na Barcelona katika kilele cha Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga baada ya kuichakaza Granada kwa magoli 4-0 na kupata ushindi wa kirahisi.

Real iliyoshusha kikosi chenye mabadiliko ya wachezaji tisa, ilikuwa bila Cristiano Ronaldo na Gareth Bale, lakini ilipata goli la kuongoza ndani ya dakika tatu na kufikisha manne katika dakika 35.

Katika mchezo huo James Rodriguez alifunga goli la kwanza akipokea pasi kutoka kwa Lucas Vazquez, kisha baadaye akafunga goli la pili kwa mpira wa kichwa kabla ya Alvaro Morata kufunga mengine mawili.
                     James Rodriguez akishangilia mara baada ya kufunga goli la kwanza
                        Alvaro Morata akiachia shuti na kufunga goli la tatu la Real Madrid
Katika mchezo wa awali Lionel Messi alifunga goli lake la 50na 51 katika msimu huu wakati Barcelona ikiifunga Villarreal kwa magoli 4-1, huku Neymar na Luis Suarez nao wakifunga goli moja kila mmoja.
                     Neymar akiwazidi maarifa mabeki wa Villarreal na kufunga goli la kwanza 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post