RIYAD MAHREZ ASEMA ANATAKA KUONDOKA LEICESTER CITY SASA

Mshambuliaji wa Leicester, City Riyad Mahrez, ametangaza kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo.

Mchezaji huyo aliyejiunga na Leicester akitokea klabu ya Ufaransa ya Le Havre kwa kitita cha paundi 400,000 mwaka 2014, amesema alikubali kubakia timu hiyo mwaka jana baada ya kutwaa ubingwa na kuongea na Mwenyekiti wa klabu.

Hata hivyo amesema anamipango mikubwa ya baadaye hivyo basi ameiarifu klabu kuwa anafiriki sasa ni wakati muafaka kwa yeye kuondoka Leicester.

Mahrez, mshindi wa Tuzo ya Wachezaji Bora wa Kulipwa kwa mwaka 2016, ameshuka dimbani mara 48 akiwa na Leicester City katika msimu huu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post