SAKATA LA VYETI FEKI LATUA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufanya ukaguzi wa vyeti vya watumishi wa umma kutokana na kile walichosema kuwa baadhi yao wanafanya kazi kinyume na utaratibu hivyo kutilia mashaka uwezo wa wa kitaaluma.
Wajumbe hao waliyasema hayo wakati wakitoa mchango katika hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Katiba, Sheria na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2017­/2018.
Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo ambaye ni Mwakilishi wa Mwanakwerekwe, Abdalla Ali Kombo alisema imefikia wakati serikali ya Zanzibar kuiga mfano wa Tanzania bara kwa jinsi walivyoendesha zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi. Katika uhakiki uliofanyika, jumla ya watumishi 9,932 walibainika kuwa na vyeti vya kughushi huku wengine zaidi ya 3,000 wakiwa na vyeti vya utata.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Magogoni, Shekh Hamad Mattar alitaka serikali kurekebisha baadhi ya sheria zake ambazo bado zina kasoro nyingi na hivyo kupelekea lawama za mara kwa mara kutoka kwa wananchi kutokana na utendaji mbovu wa watumishi wa umma.
“Bado katika sekta za ajira kuna malalamiko mengi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ili kuepukana na kasoro hizo ambazo mara nyingi huwavunja moyo wananchi wa Zanzibar,” alisema Mattar.
Ushauri wa wawakilishi umekuja ukiwa ni majuma machache baada ya Rais Dkt Magufuli kukabidhiwa ripoti ya uhakiki wa watumishi wenye vyeti feki ambapo aliamuru waondoke katika utumishi wa umma kabla ya Mei 15 mwaka huu, vinginevyo wangefikishwa mahakamani.
Aidha, tangu Rais atoe agizo hilo, watu mbalimbali wamefika katika Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kuhakiki vyeti vyao kwa kile walichodai kuwa wana vyeti halali lakini wanashangaa kutajwa miongoni mwa wenye vyeti vya kughushi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post