SERIKALI YA KUWAIT YAINGILIA UCHUNGUZI WA MAUAJI MKOA WA PWANI

Ubalozi wa Kuwait nchini umeishauri Serikali kutumia busara zaidi katika kutatua na kudhibiti mauaji yanayoendelea mkoani Pwani na kufanyika kwa uchunguzi wa kina.
Mpaka sasa tayari takriban watu 31, wameshauawa katika wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga kuanzia Mei mwaka jana wakiwamo viongozi na askari wa Jeshi la Polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari hizi, Katibu wa Kwanza wa Ubalozi wa Kuwait Mohammad Alamiri ambaye alimwakilisha Balozi wa nchi hiyo amesema kwamba watu wanaouawa Kibiti ni wale wasiokuwa na hatia.
“Tanzania ni nchi yenye amani lakini haya mauaji yanaitia doa kwa kiasi kikubwa ni vizuri uchunguzi ukafanyika ili kubaini nini hasa chanzo cha mauaji hayo ambayo yanaangamiza wasiokuwa na hatia,” amesema Alamiri.
Amesema  pia angeshauri Jeshi la Polisi kukamata wauaji halisi badala ya kuwakamata watu ambao hawakuhusika kabisa na mauaji hayo jambo ambalo linaleta hofu kwa wakazi wa maeneo husika.
Katibu Mohammad Alamiri amesema Serikali inapaswa kuwashirikisha wananchi katika kupambana na mauaji ya polisi na raia yanayoendelea kutokea katika wilaya hizo hususan kipindi hiki cha kuelekea mwezi mtukufu wa ramadhani unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post