SERIKALI YAANZA KUPATA MACHUNGU YA KUWAFUKUZA WENYE VYETI FEKI

Wakati athari za uhakiki wa watumishi walioghushi vyeti zikiendelea kujionyesha na kuzua tafrani maeneo mbalimbali, serikali imewataka waajiri katika maeneno mbalibali yalioathirika sana na operesheni hiyo kuomba vibali vya ajira vya dharura ili kutoathiri huduma kwa wananchi.
Tokea kutajwa kwa wafanyakazi wenye vyeti feki na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, hali imekuwa tata katika baadhi ya ofisi za umma, kama shirika la posta na hospitalini ambako huduma kwa wagonjwa zimeathirika.
Pia mkanganyiko umeibuka sehemu kadhaa kutokana na baadhi ya wafanyakazi kutajwa katika orodha hiyo kuanza kumiminika ofisi za baraza la Mitihani (Necta) kuhoji mustakabali wao, huku wengine wakiamua kutoenda ofisini hivyo kuathiri huduma.
Hii ni baada ya agizo la Rais John Pombe Magufuli la kuwataka wale wote waliobainika kuwa na vyeti feki kuondoka kazini mara moja kwa hiari na watakaokaidi kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumzia hali hiyo Bungeni Dodoma jana, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro alizitaka mamlaka ambazo zimeathirika sana na zoezi hilo kuomba vibali vya dharura vya ajira.
“Kuna baadhi ya maeneo yameathirika sana na zoezi hili ka uhakiki, hivyo watuandikie kuomba vibali vya ajira vya dharura ili huduma zinazotolewa zisiathirike,” alisema.
Ndumbaro alisema kuwa kuna baadhi ya watumishi waliojitokeza kuwa wana vyeti halali, lakini baadhi yao waligundulika kuwa waliwasilisha kwa waajiri vyeti tofauti na wanavyoviwasilisha hivi sasa.
Alisema kuwa wameshapokea malalamiko hayo ya vyeti kutoka kwa kwa baaadhi ya watumishi ambao wanadai wana vyeti halali.
“Kuna wawili tumewaona hadi sasa na wamewasilisha vyeti ama nakala ya vyeti vyao tofauti na vile wanavyoviwasilisha hivi sasa kwa ajili ya uhakiki. Na hawa ni wale waliochangw grade (madaraja) katika vyeti vyao” alisema.
Alisema pamoja na watumishi hao kuwasilisha vyeti hivyo kwa ukaguzi wa pili, walivitumia katika kuendelea na masomo jambo ambalo halitawaondoa katika orodha ya vyeti vya kughushi.
Pia Ndumbaro alisema watumishi ambao waliwasilisha vyeti pungufu wanatakiwakuwasilisha vyeti vyao kabla ya Mei 15 kwa ajili ya kuhakikiwa na kwamba wasiofanya hivyo, watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Jumla ya watumishi 11,596 waliwasilisha vyeti pungufu katika zoezi hilo huku 1,538 vikiwa na utata na 9,932 vikibainika kughushiwa.
Kwa mujibu wa Ndumbaro, uhakiki bado unaendelea kwa watumishi walioko Serikali Kuu na unatarajiwa kukamilika Mei 10.
Alisema wale watakaobainika kuwa wana vyeti halali baada ya kukaguliwa kwa mara ya pili, watarejeshwa katika utumishi wa umma.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post