SERIKALI YAELEZA KILICHOKWAMISHA RIPOTI MPYA YA WATUMISHI WENYE VYETI FEKI

Serikali  imesema kuwa ripoti mpya ya watumishi wenye vyeti vya kughushi waliopo katika wizara na taasisi za serikali imechelewa kutolewa ili kuepuka kasoro iliyojitokeza katika ripoti ya kwanza.
Kasoro ambayo serikali imesema kuwa inafanyakazi kwa makini kuweza kuiepuka ni kuwaorodhesha watumishi wenye vyeti kamili katika orodha ya wenye vyeti pungufu kama ilivyokuwa katika orodha ya awali ambapo waliorodheshwa aidha baada ya kuchelewa au kupuuza kuwasilisha vyeti vyao.
Hayo yalibainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurean Ndumbaro ambapo alisema uhakiki wa vyeti sasa upo katika hatua ya kuhakiki wenye vyeti pungufu ili wasiwaweke wengine kimakosa.
“Tumeshamaliza uhakiki, hatujatangaza sababu tunawahakiki waliopatikana na ‘incomplete’ (pungufu), tunataka tukimaliza tutoe majibu yasiyo na malalamiko” alisema Dk. Ndumbaro.
Dk. Ndumbaro alisema wanaweka umakini mkubwa ili mtu atakapotajwa kuwa hana cheti basi kunakuwa hakuna malalamiko kwa sababu watakuwa tayari wamejiridhisha.
Katibu huyo alisema pia idadi ya watu waliotajwa katika orodha ya wenye vyeti feki ni wachache na majina yao yatatolewa mwishoni mwa mwezi huu. Alifafanua pia zaidi kuwa, wengi waliokata rufaa ni wale waliobadili majina kwa sababu mbalimbali kama kuolewa lakini wakasahau kuwasilisha nyaraka zao.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post