SHAMBULIZI LA KOMPUTA KUATHIRI WATU ZAIDI KESHO JUMATATU

Wataalmu wa usalama katika mitandao ya komputa, wanaonya kwamba kunaweza kutokea mashambulio mengine sehemu mbalimbali za dunia, pale watu wataporudi makazini hapo kesho.
Inakisiwa kuwa komputa zaidi ya 120 katika nchi takribani 100, zilidukuliwa Ijumaa.
Lakini polisi wa Umoja wa Ulaya wanasema walioathirika ni 200,000 katika nchi 150.
Shambulio hilo limeathiri watumizi pamoja na ofisi za serikali, kampuni zinazotengeneza magari, mabenki na huduma za afya.
Shambulio hilo linazuwia komputa kufanya kazi, mpaka hapo utakapowalipa fedha ili waifungue komputa yako.
Uchambuzi uliofanywa na BBC katika akaunti tatu za sarafu ya kidijitali, bitcoin, unaonyesha washambuliaji wamelipwa pesa zaidi ya mara 100, jumla ya dola karibu 30,000.
HT @ BBC
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post