SIDIRIA YENYE UWEZO WA KUTAMBUA SARATANI YA MATITI YAVUMBULIWA

Juliana Rios Cantu, raia wa nchini Mexico mwenye umri wa miaka 18 amevumbua sidiria inayoweza kugundua saratani ya matiti.
Sidiria hiyo aliyoipa jina Eva ameitengeneza yeye pamoja na rafiki zake watatu na walianzisha kampuni iitwayo Higia Technologies.
Kampuni yao Higia Technologies iliibuka mshindi baada ya kuzishinda kampuni nyengine za biashara kutoka kote duniani ili kushinda dola 20,000 kuzalisha wazo lao.
Wazo la sidiria ya Eva ni kwamba ina sensa ambazo inaweza kupima viwango vya joto, kuviweka katika programu na kumuelezea mtumiaji kuhusu mabadiliko yanayomsumbua. Uvimbe ulio na saratani unaweza kupandisha vipimo vya joto mwilini.
Wanawake wanaohitaji sidiria hiyo watalazimika kuivaa kwa dakika 60 hadi 90 kwa wiki ili kupata vipimo vilivyo sawa.
Hii ni kwa awamu ya kwanza ya dalili za ugonjwa huo.
Tayari sidiria hiyo imefanyiwa majaribio na itafanyiwa vipimo vyengine vya kimatibabu kabla ya wataalam wa ugonjwa wa saratani kuipendekeza kuwa njia ya kugundua saratani.
Anna Perman kutoka kituo cha utafiti cha Uingereza ameeleza kuwa: “Tunajua kwamba uvimbe huo una mishipa isio ya kawaida ya kupitisha damu na tunajua kwamba kasi ya damu katika mishipa sio thibitisho kwamba mtu anakabliwa na saratani.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post