SIFA 10 ZA MUME AMBAYE HATOACHA KUKUPENDA

Ndoa ni kujikabidhi moja kwa moja kwa mwenza wako. Ndoa ni ahadi unayoiweka kuyatoa tunu maisha yako kwa ajili yake.
Hivyo, kama wataka himaya maridhawa ya aina hiyo, na unamtaka mwanaume ambaye hatokutupa mkono mambo yatakapokuwa magumu, basi zote kali blog imekuandalia sifa chache ambazo unatakiwa kuzitafuta kwa mwenza wako:

 1. AHADI YA KUSHIKAMANA NAWE NA ANAIFANYIA KAZI

Unahitaji mwanaume ambaye amejikabidhi kwako kwa asilimia 100, anayeahidi kushikamana nawe na ndoa yenu. Katika ndoa, mnaahidi kupendana daima – sio mpaka wakati wa shida. Ndoa ni muungano mtukufu kati ya roho mbili, hivyo unahitaji kuwa na mtu ambaye ni muaminifu na anashikamana na ahadi na yamini zake.

2. ANASHUGHULIKIA MATATIZO MAPEMA NA KWA UPOLE

Mwanaume wa kweli huzitilia maanani hisia zako. Akiweza kukwambia kuwa kitu fulani hakipo sawa, atakieleza. Usipoteze muda wako na yule ambaye hatorekebisha matatizo katika uhusiano wa ndoa yenu. Ndoa haiwezi kudumu bila kufanya juhudi.

3. ANA UTAYARI WA KUKUSAIDIA KUONDOKANA NA CHANGAMOTO ZAKO

Unapovurugwa, huwa yuko tayari kukusaidia kupambana na maumivu hayo – hata kama yeye sio chanzo. Kwa nini? Kwa sababu hataki kukuona ukiwa umeumia. Mzigo wako ni mzigo wake, na yuko nawe katika changamoto hizo.

4. HAPUUZI KILA JAMBO

Je, hapuuzi mambo madogo? Anaweza akawa hajui kila kitu kuhusu maisha yako, lakini anayatambua mambo unayoyajali, yanayokuhusu na unayoyapenda hata kama kwake yanaonekana kuwa ni madogo. Iwapo unapenda mawasiliano, basi hatoacha kuwasiliana nawe, iwapo unapenda busu la asubuhi hatoacha kukupatia au iwapo unapenda zawadi ya pipi na tofaa hatoacha kukuletea.

5. NI MWENYE BUSARA NA HEKMA

Ni jambo zuri kuwa na mtu maridadi, lakini ni jambo bora zaidi kuwa na mume mwenye hekma na busara, kwa sababu mwenye kupewa hekma amepewa heri nyingi. Hekma ndio nguzo muhimu inayotakiwa kushikilia ndoa, tofauti na uhusiano wa udugu. Kwenye udugu kinachohitajika ni hisia, lakini kwenye mafungamano ya ndoa tunahitaji hekma zaidi kuliko chochote kile. Hivyo ukiwa na mtu mwenye hekma linapotokea tatizo au changamoto atatafakari nama ya kuzikabili na kuzitatua.

·         6. ANAKUJUA VIZURI KULIKO UNAVYOJIJUA

Ni muhimu sana kuwa na mtu ambaye anaweza kuwaza kwa uhakika kuhusu radiamali (reaction) yako kwenye hali ngumu. Kwa namna hiyo anaweza kujua namna ya kukulinda dhidi ya radiamali, hisia hasi na jazba zinapolipuka.

7. ANAJALI MNO JINSI UNAVYOJIHISI

Haishii kuona kuwa wewe ni mzuri, bali anataka nawe ujihisi kuwa kweli ni mzuri. Unapoushusha hadhi muonekano wako, yeye anakuwa wa kwanza kukwambia kuwa unakosea.


8. ANAYAFUTA MACHOZI YAKO

Mume anaweza kumfariji sana mke kwa namna ambayo hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya hivyo. Unapopatwa na tatizo, yeye ndiye mtu anayeweza kuyafuta machozi yako. Huruma yake inaweza kusaidia kukurejeshea ari na kukupa ujasiri wa kusonga mbele. Basi unatakiwa kuwa na mtu wa namna hiyo.

9. ANAZIPA KIPAUMBELE SHIDA ZAKO

Furaha yako ni jambo muhimu kwake, hivyo unapokuwa unakabiliwa na tatizo basi tatizo hilo huwa lake pia, hulibeba. Ni muhimu kuwa na mume ambaye shida zako anazifanya kuwa kipaumbele chake. Hakuna kitu kinacholeta faraja kama kuwa na mtu anayejali sana mambo unayohangaika kuyafanya.

10. ANAZIHESHIMU TOFAUTI ZENU

Bila shaka mwanaume na mwanamke ni viumbe wawili tofauti kabisa katika ulimwengu wao wa ndani. Tofauti hizo ndizo zinazowafanya kuwa wanaume na wanawake. Kitu kikubwa sana kwa mwanandoa ni kuyaheshimu yale mambo yanayowatofautisha na kuweka mkazo kwenye yale mambo yanayowaunganisha. Hivyo, ni muhimu sana kuwa na mume ambaye anaziheshimu tofauti zenu, anaheshimu wivu wako, anaheshimu mihemko yako, na anaheshimu silika (natural instincts) zako.

Na bila shaka hakuna mtu mkamilifu--- hata wewe si mkamilifu. Lakini kumpata mtu anayekuweka mbele na kukufanya kuwa namba moja, ni ufunguo wa ndoa yenye furaha.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post