SIMBA WAONYESHA RUFAA WALIYOPELEKA FIFA KUPINGA UBINGWA WA YANGA

Klabu ya Simba imetoa kiambatanisho kinachoonyesha kuwa tayari wametuma rufaa yao Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na kwamba minong’ono inayoendelezwa mitaani kwamba hakuna cha rufaa si ya kweli.
Rufaa hiyo ya Simba wanapinga maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wa kuirejeshea Kagera Sugar alama 3 licha ya kudaiwa ilimchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano.
Taarifa iliyotolewa na Simba leo baada ya Ligi Kuu Tanzania kumalizika inasomeka hivi;
Rufaa ya Simba ilishapelekwa FIFA.
Katika siku za karibuni kumekuwa na minon`gono na upotoshaji wa habari juu ya rufaa ya Simba.
Ukweli ni kuwa, Simba imekata rufaa na ilishapelekwa kama ambavyo kiambatanisho kinaonyesha.
Uongozi unawapongeza mno Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Simba kwa sapoti kubwa kwa timu yao. Tunaamini haki itatendeka!.
Kama FIFA watatoa maamuzi tofauti na yaliyotolewa na Kamati ya TFF, Simba watakuwa ndio mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2016/17.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post