SIMULIZI YA MAISHA YA MTOTO ANAYEISHI KWA KUNYWA MAFUTA YA KULA, MAZIWA NA SUKARI

Ugonjwa ulioanza kama malaria, umegeuka na kuwa masaibu na maradhi ya ajabu kwa kijana Shukuru Mussa.
Wakati watanzania wengi wakitumia sukari kwa ajili ya chai, mafuta ya kula kwa kukaangia maandazi, chapati na kupikia mboga pamoja na vyakula vingine, hali ni tofauti kwa kijana Shukuru.
Yeye hunywa mafuta na maziwa tu. Hunywa mafuta kama yalivyo na kubwia sukari kama ilivyo. Au sukari huwekwa kwa kiasi kikubwa sana kwenye chai yake.
Baada ya kusaka tiba kwa miaka 16 bila mafanikio, saa nuru ya matarajio yake imeanza kuonekana baada ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  (MNH) kujitolea kumpatia matibabu.
Aliwasili MNH jana akitokea tunduru anakoishi akiwa na mama yake mzazi, Mwanahabibi Mtenje ambaye alisema mwanaye amasumbuliwa na taito hilo kwa muda mrefu na amehangaika bila kupata ufumbuzi kwa miaka 16.
“Nilikuwa natumia mafuta ya kula lita moja kwa siku, sukari robo tatu ya kilo pamoja na maziwa lita mbili kwa siku kama chakula chake. Nilikuwa naumia sana kwa sababu ni mjane,” alisema.
Alisema kuwa alihangaika bila mafanikio kwa muda mrefu kuhakikisha Shukuru anapona kwa kuwa hakujua mwanaye anahitaji tiba gani.
“Baada ya Shukuru kufikishwa katika hospitali hii nina imani atapata tiba zote na Mungu atamjalia kupona maradhi hayo. Nawashukuru madaktari, wamenipokea vizuri hapa Muhimbili. Ndugu zangu kokote mlipo nisikieni Mama Shukuru nimeshapokelewa hospitalini,” alisema Mwanahabibi kwa hisia.
Akizungumzia tatizo la mwanaye, Mwanahabibi alisema anapokosa ‘vyakula’ hivyo mwili wote hupata maumivu na nyama zake kujikatakata na kushindwa kwenda kokote.
“Hali hii ikimkuta akiwa shuleni analazimika kubebwa na kurudishwa nyumbani. Yaani hali ikianza ni kama gari limeishiwa mafuta,” alisema Mwanahabibi.
Hali hii ikianza anatakiwa apate vitu hivi (sukari, maziwa na mafuta) wakati wowote. Pia huwa na tabia ya kubadilika rangi mara ya njano mara bluu, halii hii ikishamkumba inabidi ale vyakula vyake,” alisema.
Meneja Uhusiano wa MNH, Aminieli Eligaesha alisema Shukuru alifikishwa juzi usiku, baaada ya Serikali kuagiza apelekwe Muhimbili kwa ajili ya maibabu.
Alisema ameshaanza kuchukuliwa vipimo ikiwamo vya damu ambayo imepelekwa maabara.
“Tunatarajia majibu yatatoka muda si mrefu, ambayo yatatuwezesha kubaini kitu kinachomsumbua,” alisema Eligaesha.
Alisema kuwa Shukuru yupo chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari bingwa wa fani zote.
Eliagesha alifafanua kuwa hospitali hiyo imechukua jukumu la gharama za matibabu hivyo mzazi wa mtoto huyo hatochangia kiasi chochote.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post