SINGIDA UNITED MDOGO MDOGO MPAKA MWANZA

Klabu ya soka Mkoani singida ambayo kwa mara ya kwanza itashiriki ligi kuu soka Tanzania Bara msimu ujao,italazimika kuuacha Mkoa wake wa Singida na kuhamia Jijini Mwanza kwa muda kufuatia kukosa uwanja wa kufanyia mazoezi, mara baada ya uwanja wao wa mazoezi wa Namfua kuwa kwenye matengenezo.

Kocha wa klabu hiyo raia wa Uholanzi, Hans van Der Pluijm kuutaka uongozi wa klabu hiyo .
Mwenyekiti wa Singida United, Yusuph Mwandami, amesema kuwa baada ya mapendekezo hayo ya Pliujm, kwa pamoja walikubaliana na ushauri huo, hivyo muda wowote mambo yatakapokuwa sawa, timu hiyo itaenda kukaa kwa muda jijini Mwanza.
Uwanja wa mazoezi wa klabu ya Singida United.
“Hata hivyo, pindi uwanja wetu wa Namfua utakapokuwa tayari, basi timu itarudi Singida kuendelea na maandalizi yake kwa ajili ya ligi kuu.
“Niwaombe tu wapenzi na mashabiki wetu, hususan wakazi wa mkoani Singida, kuwa wavumilivu katika kipindi chote ambacho timu yao itakapokuwa Mwanza,” alisema Mwandami.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post