STAA WA FILAMU ZA BONGO AFUNGUKA KUHUSU KUSUMBULIWA NA WABUNGE

STAA wa filamu za Kibongo, Mwanaheri Ahmed amesema kuwa anawatahadharisha wabunge wanaomsumbua mitandaoni na kwenye simu yake kuwa wakiendelea atawataja kwani anawaheshimu sana.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Mwanaheri alisema kuwa kutokana na shepu aliyonayo amekuwa akisumbuliwa na wabunge tofauti kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo humfuata DM na kwenye simu yake kumuomba kuingia naye kwenye uhusiano kitendo ambacho kinamhatarishia uhusiano wake na mpenzi aliyenaye sasa.
“Unajua nashindwa kuwataja wabunge wanaonisumbua kwasababu nawaheshimu lakini nimesema iwapo wataendelea nitawataja kwa sababu inakuwa kero na imewahi kuniharibia kwa mpenzi wangu mpaka kufi kia hatua ya kuniambia niondoke huko wakati huko ndiyo nafanya kazi zangu za biashara pamoja na fi lamu kwa ujumla,” alisema Mwanaheri.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post