TAARIFA KUHUSU HALI YA WANAFUNZI WA LUCKY VICENT WALIOJERUHIWA KWENYE AJALI KARATU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa watoto waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea Mei 6 eneo la Rhotia Marera, wilayani  Karatu wanaendelea vizuri.
Waziri Ummy Mwalimu ameyasema haya  leo alipotembelea watoto hao wa shule ya Lucky Vicent ambao wamelazwa katika (Mount Meru).
Akiwa nje ya wodi ya wagonjwa mahututi walipolazwa watoto hao katika Hospitali hiyo, Waziri Mwalimu aliuhakikishia umma wa watanzania kuwa majeruhi hao wanaendelea vizuri; na kuwa tayari Wizara imeshapeleka Madaktari bingwa Watatu kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) ili wasaidiane na Madaktari wa Mount Meru pamoja na wale madaktari watalii kutoka shirika la STEMM Marekani.
Waziri Ummy amewahakikishia wazazi, walezi, ndugu na jamaa wa majeruhi kuwa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, itahakikisha watoto hao wanapata matibabu sahihi ili waweze kurejea shule kuendelea na masomo.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post