TAARIFA KUHUSU RIPOTI YA KAMATI ILIYOCHUNGUZA MCHANGA WA MADINI ULIPO KWENYE MAKONTENA

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), kimesema hakijaridhika na hatua ambayo inachukuliwa na serikali chini ya Wizara yake ya Mambo ya Ndani katika kushughulikia mauaji yanayoendelea nchini na kuitakata kutafuta njia madhubuti ya kudhibiti mauaji hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga, alisema kumekuwa na matukio ya mfululizo katika kipindi kifupi hususani katika Mkoa wa Pwani, lakini mpaka sasa hawaoni njia mbadala ambayo imefanywa na serikali kuhusu mauaji hayo.
Alisema kupeleka askari wengi Mkoa wa Pwani na maeneo mengine kunakotokea mauaji hayo hakutasaidia endapo hakutafanyika uchunguzi wa kina kujua chanzo chake.
“Kinachotakiwa hapa ni kuhakikisha inatafutwa njia madhubuti ambayo itasaidia kuja na majibu ya kutatua tatizo hili, wafanye uchunguzi wa kawaida wa kijamii, kukaa na wananchi, tunaamini watapata tu sababu zake na hapo ndipo itakuwa mahali pazuri pa kuanzia na hii pia itasaidia wao kujua ni mbinu gani watumie kuwashughulikia,” alisema.
Alisema LHRC ilipeleka timu yake mkoani Pwani kwa ajili ya kufanya uchunguzi juu ya matukio hayo ya mauaji na kwamba hivi sasa wako katika hatua za mwisho za mapitio ya ripoti ya uchunguzi na itasomwa hadharani ikikamilika.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post