TAARIFA MPYA KUHUSU MTI ULIOKUWA UMEGOMA KUNG’OLEWA JIJINI MWANZA

Mti uliowaacha na mshangao mkubwa watu mbalimbali wa Jijini Mwanza kwa kudaiwa kutoa sauti kama binadamu ukipinga kung’olewa, tayari umeshaondolewa katika eneo ulipokuwa kupisha upanuzi wa barabara.
Mti huo unadaiwa kutoa sauti hiyo jana jioni katika Barabara ya Pasiansi Mwanza wakati uking’olewa kupisha upanuzi wa barabara inayokwenda uwanja wa ndege jijini Mwanza.
Baada ya taarifa hizo kusambaa, watu mbalimbali leo walikusanyika kwenye eneo hilo kuushuhudia mti huo, huko mafundi wa barabara wakiendelea na jitihada za kuung’oa.

Watu wengi waliokuwapo katika eneo hilo, na walioshuhudia tukio hilo jana, walilihusisha na imani ya kishirikina kwani jambo la kawaida kusikia mti ukizungumza.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post