TAARIFA YA MAENDELEO YA WATOTO WA LUCKY VICENT WALIOPELEKWA MAREKANI KUTIBIWA

Watoto wa tatu wa Shule ya Msingi ya Lucky Vicent ya jijini Arusha waliopelekwa nchini Marekani kwa ajili ya matibabu, wanaendelea vizuri ambapo wawili tayari wamefanyiwa upasuaji na kuonyesha maendeleo ya kuridhisha, na mmoja anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo (spinal surgery) leo.
Watoto hao, Sadia, Doreen na Wilson walipelekwa Marekani kwa ajili ya matibabu baada ya kunusirika katika ajali ya gari iliyopelekea vifo vya wenzao 32, walimu 2 na dereva mmoja, iliyotokea wilayani Karatu mkoani Arusha.
Mtoto Wilson, anayeonekana hapo juu kwenye picha juzi alianzishiwa mazoezi ya viungo (Therapy), baada ya zoezi la upasuaji kukamilika, na Madaktari wamesema kwa mara ya kwanza ameweza kukaa mwenyewe kwenye kitanda chake, na kwamba alikuwa amejawa na tabasamu kubwa.
Mtoto Sadia ameanzishiwa mazoezi ya viungo (Therapy) baada ya zoezi la upasuaji kukamilika. Madaktari wamesema mtoto Sadia kwa mara ya kwanza ameweza kusimama mwenyewe, na waliona kama muujiza na ameweza kuongea vizuri.
Mtoto Doreen (hapo juu si picha yake), juzi alipewa mapumziko maalumu siku nzima akiwa anaandaliwa tayari kwa upasuaji wa uti wa mgongo (Spinal Surgery) leo Alhamisi.(Picha kwa hisani Lazaro Nyalandu (Mb)).
Watoto hao walipelekwa Marekani kwa ajili ya matibabu ikiwa ni msaada kutoka Shirika la Kikristo la Misaada ya Kibinadamu, Samaritan Purse la Marekani. Watoto hao ndio pekee walionusurika katika ajali ya basi iliyokuwa na watu 38 walipokuwa wakielekea kufanya mtihani wa ujirani mwema wilayani Karatu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post